Kwanza: Kubainisha athari ya fikra za kimalezi kuhusu Zaharaa (a.s) katika jamii ya kiislamu.
Pili: Kuangazia maswala ya kibinadamu katika kuitambua historia ya bibi wa wanawake duniani.
Tatu: Kupata somo na mazingatio kutokana na msimamo wake (a.s) katika kupigania haki za umma na maeneo matukufu.
Nne: kupata mazingatio kutokana na hoja zake kinaoshi katika kuthibitisha itikadi kwa njia ya mazungumzo.
Tano: Kuzipamba maktaba za kiislamu kwa tafiti bora za kielimu kutokana na historia yake (a.s).
Kutokana na tangazo, mada zitakazo shindaniwa zitakua ni:
- Athari za kiitikadi na kifiqhi kwa bibi Zaharaa (a.s).
- Uwanja wa kibinadamu na mfano mkuu wa mwenendo wa bibi Zaharaa (a.s).
- Msimamo wa bibi Zaharaa (a.s) katika kupigania haki na maeneo matukufu.
- Nyenzo za kutengenezea familia kutokana na mtazamo wa bibi Zaharaa (a.s).
- Mazungumzo ya bibi Zaharaa (a.s) kuhusu turathi za uislamu.
Mashariti ya mashindano ni:
- Utafiti wako usiwe umesha wahi kuchapishwa au kutolewa na watu wengine.
- Usiwe chini ya kurasa (12) na sio zaidi ya (20) ukubwa wa maandishi uwe saizi (16) kwa hati ya (matin) na saizi (14) kwa hati ya (simplified Arabic).
- Pamoja na nakala ya karatasi uwekwe na kwenye (CD) liandikwe jina la mtafiti (muandishi) pamoja na namba ya simu na wasifu (CV) yake. Yasipo zingatiwa hayo hautashugulikiwa.
- Aambatanishe na muhtasari wa utafiti wake usiozidi maneno (300).
- Mwisho wa kupokea tafiti hizo ni: (10 Jamadil Aakhir 1438h).
- Viandikwe vitabu rejea vyeto kwa namba za rejea katika karatasi ya mwisho.
Tafiti zitumwe katika anuani zifuatazo:
Idara ya shule za Alkafeel za kidini upande wa wasichana – kituo cha Swidiqatu Twahira (a.s) Karbala – mkabala na mtaa wa Usra- barabara ya hospitali ya Husseini.
Au kwa email: Fatema14asad@gmail.com
Unaweza kupiga simu: 07602345585 au 07732840851.
Zimesha andaliwa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, ambazo ni:
- Mshindi wa kwanza milioni moja na laki tano (1,500,000) dinari za Iraq.
- Mshindi wa pili milioni moja na lakimbili na nusu (1,250,000) dinari za Iraq.
- Mshindi wa tatu milioni moja (1,000,000) dinari za Iraq.