Kwa undani zaidi kuhusu siraha hizo tuliongea na kiongozi wa makumbusho ustadh Swadiq Laazim, alikua na haya ya kusema: “Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu ina mamia ya siraha za moto (gobole na bastola) zilizo tolewa zawadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika zama tofauti, zingine zilikua za zamani na zingine wakati zinatolewa zilikua ni za kisasa, siraha hizo zimepambwa kwa nakshi na mapambo yanayo ashiria urasmi wa watu walio tengenezewa hizo siraha. Bunduki zipo za aina nyingi, miongoni mwake ni:
- 1- Qalaa: Inafanya kazi kwa kutumia utambi, na umbo lake limetengenezwa kutokana na mbao, huku bomba lake likitengenezwa kwa chuma na kutiwa aina tofauti za madini, sehemu ya juu ya bundiki hiyo imeandikwa (Ewe mwenye kukidhi haja).
- 2- Bundi ya zamani inayo tumia mawe: umbo la bunduki limetengenezwa kwa mbao iliyo tiwa madini ya aaji na Swafaaih, bomba lake limetengenezwa kwa chuma.
- 3- Bunduki ya zamani inafanya kazi kwa kutumia capsule, kitako na umbo la bundiki vimetengenezwa kwa mbao zilizo tiwa swadfu na aaji, bomba lake limetengenezwa kwa chuma na limetiwa madini.
- 4- Bunduki ya kizamani yenye risasi tano, kitako na umbo la bunduki vimetengenezwa kwa mbao na bomba na mtego wa kufyatulia risasi vimetengenezwa kwa chuma, pamoja na aina zingine za bunduki.
- 5- Kuna bunduki ndogo ndogo nyingi zilizo tengenezwa India, baadhi zimetengenezwa kwa chuma na kutiwa madini ya dhahabu.
- 6- Bundiki za jangwani: zinafanya kazi kwa kutumia utambi nazo ni miongoni mwa bunduki za zamani kabisa zilikua zikitumika mashariki ya kati na mashariki ya Asia toka karine ya kumi na moja hijiriyya.
Kuhusu bastola tulizo nazo ni:
- 1- Bastola inayo fanya kazi kwa kutumia utambi, imetengenezwa kwa mbao iliyo tiwa aaji na kupambwa kwa nakshi.
- 2- Bastola ya kizamani inatumia capsule, umbo lake limetengenezwa kwa mbao zilizo tiwa aaji, bomba lake limetengenezwa kwa chuma na kutiwa madini pamoja na kuwekwa nakshi zenye umbo la simba pamoja na aina zingine.
- 3- Bastola ya aina ya wabli inafanya kazi kwa kutumia capsule.
- 4- Bastola aina ya wabli inayo fanya kazi kwa mtego wa kufyatulia.”.
Akaendelea kusema kua: “Hadi leo bado siraha za moto zinaendelea kuzawadiwa katika makumbusho ya Alkafeel, tunazo siraha tulizo pewa zawadi na wapiganaji wa hashdi sha’abi, baadhi yake zimechovya dhahabu, miongoni mwa bunduki zilizo tolewa zawadi kwetu kuna moja ilipigana vita vitatu; vita kuu ya dunia ya kwanza na ya pili pamoja na vita vya kuukomboa mji wa Aamirili, nayo ni aina ya (burnu) imetengenezwa mwaka (1915m)”.
Kuhusu uhifadhi wa siraha hizi Ustadh Swadiq alisema kua: “Siraha hizi hutunzwa na kusafishwa na watu walio somea utunzaji wa fifaa vya makumbusho kwa kutumia kemia na vitu vya kawaida kama vile sponji na katani, na huhifadhiwa kwa njia za kitaalamu ikiwa pamoja na kuweka hewa maalumu yenye viwango vinavyo takiwa vya baridi au joto”.