Hospitali ya rufaa Alkafeel na Hashdi sha’abi wafanya makubaliano kuhusu kutibiwa kwa majeruhi..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu dokta Haidari Bahadeli ametangaza kuhusu kufanyika kwa makubaliano na madaktari wa hashdi sha’abi yanayo husu umuhimu wa kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa majeruhi wa hashdi sha’abi kupitia madaktari bingwa wa hapa nchini, itasaidia kuondoa udhia wa safari na kupunguza gharama za matibabu, pamoja na kutibu maradhi mengine pia.

Akaendelea kusema kua: “Makubaliano haya yame ungwa mkono moja kwa moja na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) pia ni miongoni mwa malengo makuu ya Ataba tukufu kuwasaidia na kusimama pamoja na wapiganaji wote (wa serikali na hashdi sha’abi) hakika watu hawa wanastahiki zaidi ya jambo hilo, malipo yamepunguzwa hadi nusu gharama jambo litakalo saidia kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa watu wengi zaidi na kwa mujibu wa makubaliano yaliyo tiwa saini na pande mbili, ambayo yanahusu kupokea wagonjwa na kuwafanyia uchunguzi pamoja na kutoa tiba, haya yatafanyika kwa mujibu wa kanuni na mawasiliano”.

Akaendelea kusema kua: “Aina za matibabu yatakayo tolewa ni pamoja na upasuaji pia kutoa huduma bora zaidi, na kuwapatia mahala pa kulala wauguzi katika hotel nzuri”.

Akafafanua kua: “Hakika madaktari wa hashdi sha’abi kuichagua kwao hospitali ya rufaa Alkafeel ni kwa sababu ya uwezo wa kimataifa uliyo nayo hospitali hii na mchango wake katika kuwatibu majeruhi wa hashdi sha’abi ambapo ndani ya mwaka uliopita tumetibu zaidi ya majeruhi (600)”.

Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel tangu kuanzishwa kwake imetilia umuhimu mkubwa msaada wa kibinadamu na kutoa kipawa mbele zaidi kwa majeruhi wa hashdi sha’abi, wengi wamefanyiwa uchunguzi na kutibiwa huku wengine wakifanyiwa upasuaji kutokana na mazingira yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: