Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua mtandao wa kijamii kwa wanafunzi wa shule za upili..

Moja ya vipengele vya programu
Miongoni mwa harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni harakati za kuwasiliana na rika zote katika jamii, na imeweka vipawa mbele vyake, na kilicho muhimu zaidi ni tabaka la wanafunzi wa ngazi za awali, kwa sababu wao ndio msingi ambao juu yake hujengwa jamii, na miongoni mwa ratiba hizi ni ile ya mawasiliano na ya kielimu na kutambuana inayo simamiwa na idara ya harakazi za shule, ambayo ipo chini ya idara ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inahusisha kualika wanafunzi wa shule za upili (O levo na A levo) na kuwaingiza katika programu iliyo andaliwa hapo kabla, inalenga kukuza uwezo wao wa akili na maarifa na kwa namna nyingine ni sehemu ya kujiburudisha na kupumzisha akili kutokana na uchovu wa darasani.

Ustadh Haidari Karim Kaadhim kiongozi wa idara ya harakati za shule alisema: “Programu ya kuwaunganisha wanafunzi wa shule za upili (sekondari) za mkoa wa Karbala tukufu, inalenga kuchangia uelewa wa wanafunzi na kuwafanya wayatambue zaidi mambo yanayo wakwaza katika kutafuta elimu, pamoja na mambo mengine mengi yenye uhusiano na mwanafunzi”.

Akaendelea kusema kua: “Programu hii hufanywa baada ya kuwasiliana na idara za shule kupitia ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala tukufu, huchaguliwa idadi ya wanafunzi kutokana na mazingira ya kijografia katika kila mji, kwa ajili ya urahisi wa kuwapeleka katika jengo la Shekh Kuleini (q.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Program inahusisha:

Kwanza: Kutolewa kwa mihadhara ya kidini kulingana na umri wa wanafunzi na uwezo wa uwelewa wao, ambapo huzungumziwa zaidi changamoto na hutolewa kwa njia rahisi inayo kubalika na kueleweka kwao, ikiwa ni pamoja na kujibu maswali na kusherehesha mambo yanayo wakwaza.

Pili: Kusimamisha swala ya jamaa na kubaini usahihi wa swala ya kila mmoja wao.

Tatu: Kuwafundisha udhu sahihi.

Nne: Kuwafundisha kisomo sahihi cha Qur an tukufu hasa sura zinazo somwa katika swala.

Tano: Mihadhara kuhusu maendeleo ya binadamu, inayo endana na mazingira ya wanafunzi, na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao kama yapo shuleni au nyumbani.

Sita: Kuitambulisha kwao Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake kwa kuwatembeza katika miradi hiyo kulingana na muda utakavvyo ruhusu.

Saba: Kujenga moyo wa uzalendo na kuipenda nchi, kwa kuwakumbusha ubora wa nchi hii tukufu na mema iliyo fanya kwa binadamu ili kuwafanya wajifaharishe kwa nchi yao.

Nane: Kuna vipengele vingine vinavyo husu malengo haya huingia kwa ajili ya kuboresha programu hii”.

Mwisho alisema kua: Tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wanao shiriki programu hii, tunatarajia manufaa ya programu ya akisi katika maisha ya mwanafunzi shuleni na nyumbani, na tuna mambo mengine tutayaongeza katika programu hii hivi karibuni inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: