Ugeni wa juu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika hafla namba tatu ya uzinduzi wa bandari ya Abuu Fuluus iliyopo kilometa (20) kusini mwa mji wa Basra baada ya kukamilika kwa ujenzi wake, hafla ilisimamiwa na shirika la bandari la taifa kwa kuzingatia kua ni moja ya miradi ya uzalishaji inayo fanywa na wizara ya uchukuzi ya Iraq, ugeni wa Atabau Abbasiyya umeshiriki kama wadau wa usafirishaji kutokana na mchango wao katika hilo.
Hafla ya uzinduzi imepata muitikio mkubwa kutoka kwa viongozi wa kidini, kitamaduni na kisiasa miongoni mwao; waziri wa uchukuzi, muheshimiwa Kaadhim Fanjaani Hamaami, katika khutuba yake alisema kua: “ Hakika mradi wa bandari ya Abuu Fuluus ni wa uzalishaji, utachangia katika kuongeza uchumi na utendaji wa bandari za Iraq, na mimi naelekea zaidi katika miradi ya kiuchumi hususan kuhusu mali za Iraq, naamini kua itabunguza udhia kwa wafanya biashara wa kanda hii, ukizingatia kua bahari ina nafasi kubwa katika ukanda wa waarabu”.
Akaendelea kusema kua: “Hapo nyuma tulikua hatuwezi kuingiza bidaa kwa kupitia ukanda huu, leo mbele yetu kuna meli zimebaba shehena za chakula na bidhaa zingine nyingi zinaingia katika bandari, pia jana tuliwasiliana na wafanya biashara tukawaambia wanaweza kuingiza bidhaa kupitia bandari, pia kubeba bidhaa za chakula kupitia bandari ya Abuu Fuluus”.
Nao ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulitoa pongezi nyingi kwa wasimamizi wa mradi huu mkubwa wa kiuchumi utakao changia kutoa huduma bora kwa wafanya biashara wa Iraq na kuwataka waendelee na msimamo huu.
Kumbuka kua sehemu ya kutokea inaurefu wa mita (250) upande wa maji na mita (176) upande wa nchi kavu huku ikiwa na upana wa mita (18) katika matengenezo ya sasa yalijumuisha kuibadilisha sehemu hii kutoka chuma na kupatengeneza kwa zege, na kujenga nyumba ya ofisi pamoja na kupadilisha vigingi, kujenga uzio, kuweka milango na madirisha ikiwa ni pamoja na kutengeneza njia za maji ya nvua, pia imeanzishwa idara maalumu ya kusimamia ujenzi wa zege na kufanya ukarabati kila utakapo hitajika pamoja na kuongeza upana wa eneo hili kwa mita tano.