Maahadi ya turathi za mitume (a.s) yaonyesha vikwazo vya kisheria na njia zifaazo kufanyiwa kazi..

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (masafa) iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea kufanya makongamano kutokana na makundi ya kijamii na tafiti zao kielimu, baada ya kufanya makongamano yaliyo husu masomo na kujadili changamoto za kielimu hapa Iraq hii leo wanafanya kongamano lingine kwa kundi la watu wengine, ambalo umuhimu wake ni sawa na yale yaliyo pita, nao ni tabaka la wasomi wa sheria (watoa haki), katika kongamano hili la kwanza lina wahusu wanasheria wa mkoa wa Dhiqaar chini ya anuani isemayo: (Wanasheria baina ya giza lililopo na matarajio ya kesho) kongamano la aina hii tunatarijia litafanyika katika mikoa mingine pia kutokana na ratiba ya Maahadi.

Kongamano limefanyika ndani ya ukumbi wa imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na limepata mahudhurio makubwa ya wanasheria wa mkoa wa Dhiqaar ikiwa ni pamoja na Qadhi wa mkoa na mwanasheria wa mkoa pamoja na wasomi wa kisekula, pia ilihudhuria idadi kubwa ya wakuu wa vitengo vya Ataba na idara zake, wakiongozwa na katibu wao mkuu muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) ambaye alipata nasasi ya kuongea na miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika anaye wanufausha watu hususan katika zama hizi, atapata hadhi na heshima kubwa tofauti na asiye saidia watu na anaye vunja jamii hakika mtu huyo ni sawa na povu ambalo huisha mara moja”.

Akaendelea kusema kua: “Kutokana na umuhimu wa kazi yenu katika zama hizi, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (masafa) imeamua kufanya kongamano hili, kwa ajili ya kuangalia vikwazo na matatizo mnayo kutana nayo katika kazi yenu, na kubainisha umuhimu wa jukumu lenu na kuangalia njia stahili za kutatua matatizo ya kisheria, kwani nyie ni wasimamiaji wa sheria ambazo ndio nguzo kuu katika kulinda nchi na kuhakikisha haki inatendeka”.

Akaendelea kusema kua: “Ni masikitiko makubwa sana kukuta mtu anafanya kazi hii kinyume na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mbali na ubinadamu, tunategemea kongamano kama hili iwe ni fursa kwenu ya kuongea matatizo mnayo kumbana nayo na kujadili mustakbali wenu, ili wote kwa pamoja tuunganishe nguvu katika kutatua matatizo yenu”.

Mkuu wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) Shekh Hussein Turabiy alisema kua: “Hili ni kongamano la kwanza chini ya anuani ya (Wanasheria baina ya giza lililopo na matarajio ya kesho), hawa ni tabaka la watu wenye umuhimu mkubwa katika jamii, wao ni wasimamizi wa sheria na ndio watetezi wa haki za watu au wapotezaji wa haki za watu, tukaona ni muhimu kua na kongamano kama hili, ili tuzungumzie mambo yanayo husu utekelezaji wa majukumu yao na kuelezea wajibu wa kisheria walio nao (wana sheria), itasaidia kuwafanya wahisi jukumu lao kisheria hali kadhalika matakwa ya kisheria pale walipo hitimu masomo yao na kuapa kua watasimamia sheria na kuitetea kwa uaminifu, tukaona ni vituri tukutane na watu hawa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Mwalimu wa sheria aliye wakilisha wanasheria walio shiriki katika kongamano hili alisema kua: “Tunashukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya kongamano hili maalumu la wanasheria na kuuteua mkoa wetu wa Dhiqaar, mwanasheria; ni tamko linalo jumuisha, wakili, qadhi, walimu wa sheria na kila aliye pata digrii ya kwanza (bachela) la sheria. Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kufanya kongamano hili kwa wanasheria wa mkoa wa Dhiqaar kwa kuzingatia kua ni sawa na mikoa mingine ina tatizo kubwa la maswala ya kisheria kwani kuna mambo mengi bado hayajatungiwa sheria na bunge”.

Akaendelea kusema kua: “Tunatamani bunge litunge sheria rasmi za mkoa wa Dhiqaar na waangalie mahitaji ya kisheria kwa kila mkoa, na tunatarajia kongamano hili uwe ni mwanzo wa makongamano mengine mfano wa hili”.

Kongamano hili lilikua na wazungumzaji wengi, na wote walizungumzia mazingira ya wanasheria katika maeneo ya kazi na namna ya kupambana na changamoto wanazo kutana nazo, miongoni mwa walio zungumza ni; dokta Muhammad Thaamir, Ustadh Ally Jalil, kiongozi wa wanasheria katika mkoa wa Dhiqaar Ustadh Haazim Jabaar Alkinani, pia kulikua na ujumbe wa umoja wa wanasheria ulio wasilishwa na Ustadh Abbasi Sukri Swarifi.

Kongamano lilikhitimishwa na kutoa nafasi ya kuandaa kongamano kama hili katika mikoa mingine, kisha zikatolewa zawadi na vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: