Wataalamu wa Alkafeel watoa kundi la nane la wahitimu wa huduma za uokoaji vitani..

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel katika maswala ya uokozi vitani walio chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu walikhitimisha kozi ya kundi la nane katika maswala hayo siku ya Juma Mosi baada ya adhuhuri (29 Rabiuthani 1438h) sawa na (28 Januari 2017m) katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) kozi iliyo pewa jina la (Hema la bibi Fatuma Zaharaa a.s).

Kozi ilihusu namna ya kuokoa majeruhi ndani ya uwanja wa vita, washiriki walikua 15 ambao ni wapiganaji wa kikosi cha tisa katika hashdi sha’abi na ilichukua siku saba, ilihusisha masomo ya nadhariya na vitendo, na ilifanyika katika jengo la Shekh Kuleini (r.a) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ilihudhuriwa na wapiganaji wa hashdi sha’abi kutoka katika vikosi tofauti pamoja na walimu wa chuo kikuu cha Baabil na ilifunguliwa kwa Qur an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa mwibo wa taifa na kufatiwa na mwimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha ukafatia ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio somwa na Shekh Kamaal Alkarbalaai, miongoni mwa yaliyo semwa ni: “Hakika mwanadamu anapokua katika jihadi hua chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu mtukufu na mtume wake (s.a.w.w) na jihadi sio kubeba siraha pekeyake, bali ni kila kinacho changia uwezekano wa kuendelea kwa jihadi pamoja na swala la kuwaokoa majeruhi katika uwanja wa vita, hakika swala hili linahitaji moyo na imani sahihi, tukiwa katika ugeni wa mwenye wema Abulfadhil Abbasi (a.s) tunawaambia washiriki wa kozi hii, hongereni sana kwa kushiriki kazi hii tukufu ambayo inatuletea heshima na utukufu wa dini yetu”.

Akaendela kusema kua: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawafikishe katika kufanya hii kazi tukufu, kila wakati mtakao muokoa majeruhi mtakua mnatengeneza uhai na kudumisha nusra, hivyo tunawaomba wataalamu wa kozi hii kuongeza juhudi zaidi katika kutoa mafunzo haya kwa sababu yana manufaa makubwa kwa wanadamu na yananusuru dini”.

Kisha ulifata ujumbe wa wataalamu wa Alkafeel katika maswala ya uokozi vitani ulio somwa na mganga mkuu wa sekta hiyo daktari Usama Abdulhassan akasema kua: “Hakika wataalamu wa Alkafeel ni mbegu iliyo patikana ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kupatikana dharura ya kuwaokoa majeruhi vitani, kutokana na umbali mkubwa kati ya sehemu za mapigano na magari ya wagonjwa”. Akaendelea kusema kua: “Hakika kikosi hiki kimesha fundisha zaidi ya watu (300) katika kozi za nyuma, wahitimu wetu wamefanikiwa kuokoa mamia ya majeruhi kutokana na taarifa za nyuma”.

Kisha alizungumza mshauri mkuu wa chuo cha Baabil dokta Abbasi Hussein ambaye alizungumzia umuhimu wa kozi hizi za kuokoa majeruhi, akafafanua maendeleo makubwa yanayo patikana kutoka kozi hadi kozi nyingine hususan mambo yanayo husu kuchunga muda na mazoezi ya nadharia na vitendo.

Pia kulikua na ujumbe wa wahitimu ulio wasilishwa na Muhammad Twaha Abbasi kwa niaba ya wenzake, waliishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuendesha kozi hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zina changia kuokoa maisha ya mamia ya majeruhi, akafafanua faida kubwa na uzoefu wa kutosha walio pata katika kozi hii.

Kisha ikaonyeshwa filamu iliyo rekodiwa katika mafunzo yao inayo onyesha sehemu zote mbili za kozi, sehemu ya nadhariya na vitendo, halafu wakafanya onyesho la uokozi ndani ya ukumbi, mwisho vilitolewa vyeti na midani kwa wahitimu wa kozi, vyeti walivyo pewa vinakubalika kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: