Tawi la Maahadi ya Qur an tukufu katika mji wa London lafanya nadwa kuhusu imam Mahadi na zama za kudhihiri..

Sehemu ya nadwa
Miongoni mwa harakati za kielimu na kitamaduni, tawi la Maahadi ya Qur an tukufu lililo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya nadwa kuhusu imamu Mahadi (a.f) katika Qur an tukufu huko London, mijadala iliangazia aya zinazo zungumzia kudhihiri kwa imamu Mahadi (a.f) na baadhi ya alama zake, pia zilitolewa dalili za riwaya za tafsiri zilizo pokewa kutokana na njia ya watu wa nyumba ya mtume (a.s) na zinginezo, alikaribishwa katika nadwa hii mwanachuoni mkubwa na mtafiti wa kiislamu Sayyid Muhammad Ally Halu mmoja wa walimu wa hauza ya Najafu tukufu, na kiongizi mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha.

Muandaaji wa nadwa hii na msimamizi mkuu ni kiongozi wa kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha katika Atabatu Abbasiyya tukufu shekh Dhiyaau Dini Zubaidiy ambaye aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Nadwa ni miongoni mwa harakati za tawi la Maahadi ya Qur an katika jiji la London, ambapo hualikwa watafiti na walimu wa hauza (vyuo vya kielimu) na kufaidika kutokana na elimu zao na michongo yao ambayo inahusu nafasi ya Qur an tukufu na uhusiano wake kwa watu wa nyumba ya mtume (a.s), ni nadwa ambazo huhusisha waislamu wote wanaotaka kushiriki katika mijadala ya kielimu ambapo hutolewa mada za kitafiti kwa namna ambayo hunufaisha tabaka zote, na kwa uwasilishaji unao eleweka na kila mtu, usio kuwa na taasubu (chuki za kimadhehebu) uwasilishaji unaopambwa na aya za Qur an tukufu na hadithi za mtume pamoja na riwaya za watu wa nyumba ya mtume (a.s)”.

Zubaidiy akaendelea kusema kua: “Mahudhurio yalikua mazuri sana, walimu na watu muhimu katika maswala ya Qur an wanaume na wanawake walijitokeza kwa wingi, muheshimiwa Sayyid Halu alisikiliza maswali yao kisha akawajibu na kusherehesha yaliyo hitajia kushereheshwa”.

Mwishoni mwa nadwa washiriki walitamani kuongezeka kwa nadwa za aina hii na kualikwa kwa wasomi wakubwa wa dini kama hawa ili tunufaike na hazina ya elimu waliyo nayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: