Kuthibitisha mawasiliano ya kielimu na kitamaduni: Kituo cha Ameed cha kimataifa cha tafiti za masomo chapokea ugeni kutoka katika kituo cha turathi za Samaraa kwa ajili ya kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa kushirikiana..

Sehemu ya ziara
Ugeni kutoka kituoa cha turathi za Samaraa kilicho chini ya Atabatu Askariyya tukufu ukiongozwa na mkuu wao Ustadh Mushtaaq Abdulhayyi Asadiy, umetembelea kituo cha Ameed cha kimataifa cha tafiti za masomo kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katika kikao cha ugeni huu alihudhuria pia rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Lithi Mussawiy (d.t), tulijadiliana kuhusu shughuli zinazo fanywa na kituo cha Ameed na machapisho yake pamoja na miradi yake ya baadae ambayo imesha pangwa kushughulikiwa, hali kadhalika msaada unaotolewa na kituo cha Alkatheel katika makongamano yaliyo fanywa katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ikiwa ni pamoja na kujadiliana namna ya kushirikiana baina ya vituo hivi viwili, ugeni wa kituo cha turathi za Samaraa ulikabidhi taarifa ya kituo pamoja na harakati zake katika uandishi na uhakiki na kila kilicho andikwa kuhusu turathi za Samaraa pamoja na ushirikiano wake na taasisi za kitamaduni na kielimu, pia walielezea miradi wanayo tarajia kuitekeleza ukiwemo mradi wa maktaba kubwa katika Atabatu Askariyya tukufu na jarida, pamoja na miradi mingine inayo hudumia Ataba tukufu.

Mwishoni ugeni ulionyesha furaha kubwa kutokana na harakati zinazo fanywa na kituo cha Ameed cha kimataifa katika nyanja ya elimu zinazo nufaisha tabaka zote za watu na kujenga tafakuri bora katika jamii.

Kumbuka kua ziara hii ni sehemu ya kuenzi harakati za nyuma na kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya vituo hivi viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: