Kwa picha: kuendelea kwa kazi za mradi wa upanuzi wa maqamu ya imamu Mahadi (a.f)..

Sehemu ya kazi
Chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, mafundi na wahandisi wanaendelea na kazi za upanuzi wa maqamu imamu Mahadi (a.f) kama ilivyo pangwa kutokana na ramani yake na makadirio ya muda wa utekelezaji, pia kwa usanifu bora wenye mapambo ya kiislamu na alama za turathi kwa ujumla.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh aliiambia Alkafeel ilipo tembelea mradi huo kua: “Hakika mradi unaenda kama ulivyo pangwa, shirika linalo tekeleza mradi huu (shirika la aridhi tukufu la ujenzi) linamaliza hatua moja baada ya nyingine kama ilivyo pangwa, hadi hivi sasa wamesha maliza baadhi za sehemu za mradi huu, wamesha weka zege pande mbili za mto wa Husseiniyya, kwani upanuzi unajumuisha kufunika mto na jengo litafika hadi sehemu ya mto, pia yamewekwa madaraja ya zege mengine yanayo endana na upanuzi huu, baada ya hapo; zimewekwa nguzo kutokea katika zege la ukingoni mwa mto, na tayali kazi ya kumwaga zege la juu (la dari) imesha anza na itakamilika siku chache zijazo”.

Akaendelea kusema kua: “Kazi zingine zinaendelea vizuri pia, kuna nguzo zingine ambazo zimewekwa katika awamu hii ya kwanza, ifahamike kua mradi umegawanywa katika sehemu tofauti, sehemu ya kwanza imehusisha ukumbi wa wanawake ambao unaukubwa wa mita za mraba (490) na sehemu ya pili inahusisha ukumbi wa wanaume ambao unaukubwa wa mita za mraba (310) na sehemu nyingine ni ya wahudumu wa maqamu ambayo inaukubwa wa mita za mraba (150) na sehemu nyingine ni ile ya vyoo na ndio inayo endelea kujengwa hivi sasa, ujenzi huu unafanyika katika sehemu ya muinuko wa urehu wa mita sita”.

Kumbuka kua; maqamu ya imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto Husseiniyya unapo ingia Karbala kwa njia inayo pitia maqamu imamu Jafari Swadiq (a.s) napo ni mahala mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kuikarabati upya na ilianzia katika ukarabati wa kubba na inaendelea hadi katika kumbi za haramu na sehemu zingine, kwa kua haiwezekani kufanya upanuzi wa pande tatu tu, imelazimika kufanya upanuzi upande wa mto Husseiniyya pia ambao ni upande wa magharibi ya maqamu, upo pembezoni mwake, zimewekwa nguzo za zege na juu yake yamewekwa madaraja bila kuzuia wala kubadilisha njia ya maji, kwa ukubwa unao kadiriwa kufikia mita za mraba (1200) na zimeonganika na maqamu kwa kupitia milango maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: