Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chafanya ukarabati wa njia za maji ya mvua katika eneo linalo zunguka Atabatu Abbasiyya kwa nje..

Sehemu ya kazi
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kukarabati njia za maji ya mvua katika eneo linalo zunguka uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa nje, wanaweka mabomba mapya yenye uwezo mkubwa tofauti na yazamani.

Mwanzoni mwa kazi hii ulifanyika uchunguzi wa kubaini sehemu zenye matatizo na zinazo kaa maji bila kutembea au kutembea taratibu kisha ukafanyika usanifu wa namna wa kukarabati maeneo hayo na zikapendekezwa zana zitakazo tumika na mambo mengine ya kiufundi.

Kazi hii imejumuisha kufunguliwa kwa njia mpya za maji za duara na za kunyooka inategemea na sehemu bomba linapo pita, kisha zimefunikwa vizuri na sehemu yanako pita hayo mabomba zimetengenezwa kua sehemu za ukaguzi kwa ajili ya kupunguza msongamano wa watu, njia za maji haya zinaungana na njia kuu ya kusambaza maji katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi hii imegawanywa na kufanywa kwa utaratibu ambao hauathiri kabisa shughuli za watu wanaokuja kufanya ziara.

Tunapenda kusema kua; kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo hai na chenye kazi nyingi, kina idara na ofisi nyingi pamoja na watumishi mafundi na wahandisi wanao fanya kazi usiku na mchana, katika vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ya kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwa watu wanaokuja kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: