Atabatu abbasiyya tukufu yagawa misaada kwa familia za mashahidi katika mkoa wa Dhiqaar..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba za kutoa misaada kwa familia za mashahidi na majeruhi, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ugeni wake ulioenda katika mkoa wa Dhiqaar na kugawa misaada kwa zaidi ya familia 250 za mashahidi wa jeshi la serikali na hashdi sha’abi, kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza swala hilo linalo saidia kudumu kwa vita, na kuwatia nguvu wapiganaji katika viwanja vya mapambano dhidi ya magaidi wa kidaesh, ziara hii imechukua siku mbili, vimefikiwa vijiji vingi katika mkoa wa Dhiqaar, hii ni sehemu ya ziara zitakazo fanywa katika mikoa mingine pia.

Mjumbe wa ugeni huo shekh Majidi Sultani kutoka katika kitengo cha dini aliiambia Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na ratiba yake ya kuzikirimu familia za mashahidi watukufu, ziara ya awamu hii imefanyika katika mkoa wa Dhiqaar, kama mnavyo fahamu lengo kuu la ziara hii ni kutembelea familia za mashahidi na kusikiliza shida zao pamoja na mahitaji yao, na kuwapatia misaada mitogo kwa muonekano wake lakini ni mikubwa kimaanawiyya, kwani zimetoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s). ziara hii imechukua siku mbili, siku ya kwanza tulizikirimu familia za mashahidi katika chuo cha Imam Swadiq (a.s), kisha katika siku hiyo hiyo tukaelekea katika eneo la Suuqi Shuyuukh (soko la wazee) huko tukakirimu kundi la familia zingine, siku ya pili tulitembelea mtaa wa Shuhadaau (Hayyi Shuhadaau) na tukazikirimu familia katika Jaamia Husseiniyyatul Muhsin”.

Kwa upande wao.. familia za mashahidi waliithamini sana ziara hii pamoja na takrima (zawadi) waliyo pewa, wakasema kua ziara hii ni jambo kubwa sana kwao, na inawatia moyo zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: