Kwa mara ya kwanza hapa Iraq: Darulkafeel yachapisha tafsiri ya Qur’an tukufu kwa lugha ya kijerumani na yasisitiza kua imeendana na machapisho ya kimataifa..

Moja ya kurasa za tafsiri
Darulkafeel ya machapisho na usambazaji chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa kuchapisha tafsiri ya Qur’an tukufu kwa lugha ya kijerumani iliyo fanyiwa uhakiki, itakua pamoja na msahafu wa kiarabu kwa usanifu wa kiiraq na kwa kutumia zana za kisasa kabisa katika uchapaji, kwa uchapaji bora wa kimataifa na unazidi baadhi za machapisho katika baadhi za fani, kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa machapisho Ustadhi Farasi Ibrahim.

Alisema kua: “Bidhaa za machapisho ya Alkafeel –tunamshukuru Mwenyezi Mungu- zimekubalika sana ndani na nje ya Iraq, kutokana na kutimiza vigezo vya fani za uchapaji, kutokana na hilo; wataalamu wake wameanza kuchapisha tafsiri ya Qur’an tukufu kwa lugha ya kijerumani, hili tumelipa umuhimu maalumu, kwani itagawiwa Ujerumani, hili ni jambo zuri kwa wataalamu wa kiiraq”.

Akaendelea kusema kua: “Tafsiri inayo chapishwa ni ya Sayyid Muhammad Hussein Faatwimiy, ruhusa ya kutafsiri imetoka kwa Ayatullah Shekh Makaarim Shirazi (d.dh) iliwahi kuchapishwa siku za nyuma, kwa kiwango cha chini, baada ya kuipitia nakala ya zamani ilifanyiwa marekebisho na kusanifiwa upya, walipo ipitia tena wanufaika waliipenda sana na waka afiki ichapishwe ndipo kazi ya kuichapa ilipo anza, nayo ina hatua nyingi; ikiwema hatua ya uhakiki kwa kuisoma zaidi ya mara moja kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho”.

Akaendelea kusema kua: “Tafsiri hii inasifa nzuri nyingi miongoni mwake ni:

Kwanza: Karatasi zake ni za kifahari na zina ubora wa kimataifa.

Pili: Idadi za kurasa za tafsiri hii ni sawa na idadi ya kurasa za Qur’an tukufu ambazo ni (604).

Tatu: Sura zote za Qur’an pamoja na tafsiri zake zipo katika karatasi moja, kwa namna ambayo msomaji anaweza kusoma Qur’an na tafsiri yake wakati mmoja.

Nne: Rangi nzuri na inapendeza katika macho.

Tano: Mapambo yanayo zunguka sura za Qur’an yanafanana na mapambo ya dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na yameongezewa tafsiri.

Sita: Karatasi za nakala ya zamani zilikua na ukubwa wa (A5) huku karatasi za hii nakala mpya zina ukubwa wa (A4) na ni nusu ra idadi ra karatasi za nakala ya zamani, pia zinabebeka na kusomeka kwa urahisi.

Saba: Muonekano mzuri wa uchapaji, herufi zinaonekana vizuri pamoja na uchache wa kurasa.

Nane: Uwepesi wa kufungua kitabu.

Tisa: Tafsiri imejaladiwa kwa matirio ya ngozi ambapo ni imara na zuri.

Kumbuka kua; kuanzishwa kwa mradi wa Darulkafeel ya uchapishaji na usambazaji ni miongoni mwa plani ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuhakikisha inajitegemea katika kila sekta, na kuifanya iwe na uwezo wa kutosha wa kuchapisha vitabu, majarida na nyaraka, kwa namna ambayo itamsaidia muandishi na msambazaji, vifaa vya uchapaji tulivyo navyo vina ubora wa kimataifa, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi zingine kwa vitabu, majarida na machapisho mengine.

Kwa mawasiliano zaidi na Darulkafeel ya uchapishaji na usambazaji, unaweza kutembelea ofisi zetu zilizopo katika mji wa Karbala tukufu, barabara ya Ibrahimiyya, au piga simu katika namba zifuatazo:

009647823950890

009647706733834

009647602335433
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: