Kwa vigezo vya kitafiti na kielimu: yamechapishwa majarida mengi yalo zama katika elimu na hekima..

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaati kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha majarida yaliyo shehena elimu na hekima, nalo ni jarida lenye namba za usajili wa kimataifa wa kimtandao (2312-5721ISSN) jarida hili lina juzuu moja ambalo ni juzuu la tatu na lina aina tofauti za masomo, miongoni mwa masomo yaliyomo ni: (Fizikia, Kemia, Elimu ya viumbe hai, (Biology) Hesabu, Uhandisi wa majengo na Tanakilishi (Computer)).

Jarida lina mada kumi na nne ambazo zimegawika sehemu mbili, saba (7) zimeandikwa kwa lugha ya kiarabu na saba (7) zingine kwa lugha ya kiengereza, kwa ajili ya wasomaji wa kisekula ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa uwasilishaji wa kitafiti unaokidhi vigezo vilivyo wekwa na kituo cha Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaati katika jarida hili, kuhusu fani zingine (Elimu ya mazingira na uhandisi) ambazo bado zinafanyiwa kazi na kamati ya ushauri na ya uhariri ya jarida hili kwa ajili ya kupokea tafiti za wataalamu wa kisekula wa nchini, nchi za kiarabu na duniani kote kila mmoja ataandika kutokana na fani yake aliyo bobea, ili kutoa chapisho bora kielimu lililojaa fani tulizo taja hapo juu kwa lugha mbili ya kiarabu na kiengereza.

Kumbuka kua jarida hili limeanzishwa kwa lengo la kukuza mawasiliano kati ya wataalamu wa kiiraq walio bobea na watafiti kutoka katika vyuo mbali mbali na vituo vya kielimu. Ili kuendelea kuinua kiwango cha elimu cha watafiti wetu na kuwafanya washirikiane bega kwa bega katika tafiti zao za kielimu, na kuweka mazingira ya kushindana kitafiti, na kulifanya jarida kua chemchem ya elimu za aina tofauti tena katika kiwango cha kimataifa yakiwemo maswala ya kimazingira na kihandisi, na lengo ni kuamsha akili za wanasekula katika masomo wanapo fanya tafiti za kielimu zinazo fata kanuni za kitafiti kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: