Mradi wa nyumba za kitamaduni na kimasomo wa kwanza na watatu: kazi inaendelea na kitengo cha miradi ya kihandisi chasisitiza kua itafanyika kwa viwango vya kimataifa..

Sehemu ya utekelezaji wa mradi
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesisitiza kua mradi wa majengo ya kitamaduni na kimasomo wa kwanza na watatu ni miongoni mwa miradi inayo tekelezwa kwa viwango vya kimataifa, bali unazidi hata viwango vya kimataifa katika baadhi za sehemu, kama vile upande wa usanifu na utekelezaji umetumika ufundi wa kihandisi wa hali ya juu ambao unaendana na utekelezaji wa miradi kama hii, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu mtukufu, tunatarajia majengo haya pindi yatakapo kamilika yatakua ya aina yake, kutokana na usanifu mzuri uliofanyika na namna mitambo itakavyo fanya kazi.

Akaendelea kusema kua: “Mradi unaendelea kutekelezwa chini ya shirika la (Almajmuuatul baldaawi litijaaratil a’amah walmuqaawalaat) nalo ni miongoni mwa mashirika yenye uzoefu na uwezo mkubwa, mradi huu unajengwa katika barabara ya (Karbala – Huru) katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (2m45,000), mradi unaendelea vizuri hadi sasa umekamilika kwa kiasi ya (%15) pamoja na ukubwa wa eneo na wingi wa vitengo vyake bila kusahau ukata wa pesa unao ikumba nchi kwa sasa, na kuathiri kwa kiasi utekelezaji wa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lakini kutokana na juhudi pamoja na ikhlasi ya watu wetu hatujashindwa kuendelea na utekelezaji wa mradi, na tutajitahidi kukamilisha mradi huu mkubwa ambao utaunufaisha mkoa wa Karbala na watu wake”.

Akaendelea kufafanua kua: “Kazi za mradi huu zimegawanywa katika hatua tofauti, mradi unahusisha ujenzi wa shule tano, kila moja enoe lake lina ukubwa wa mita za mraba (6,000) shule hizi zitawekwa vifaa vya kisasa vinavyo boresha mazingira ya kusoma, vifaa hivyo havijazoeleka hapa Iraq, kutakua na tanakilishi (computer) zitakazo wekwa program za huduma mbali mbali na majengo yatakua ya ghorofa tatu”.

Akaendelea kusema kua: “Mradi huu unahusisha shule mbili za watoto (Raudha) katika majengo ya ghorofa tatu yenye ukubwa wa mita za mraba (900) pia zitawekwa kila zana zinazo saidia makuzi ya akili za watoto, na kuwaandaa kwa ajili ya masomo yajayo kwa kutumia njia za kisasa, mradi huu pia unahusisha kumbi mbili za michezo, kila mmoja una ukubwa wa mita za mraba (900) ambazo zitatumiwa na wanufaika wa miradi hii”.

Akasema kua: “Mradi haujaishia katika mambo hayo tu, kutokana na ramani; kuna kituo cha kitamaduni ndani ya majengo haya ambacho kina nafasi kubwa katika mradi huu, litakua jengo la ghorofa tano litakalo jengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba elufu kumi na tano (15,000) litakua na kumbi pamoja na maeneo mengine yatakayo tumika kama kitega uchumi kutokana na itakavyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: