Kiongozi wa kikosi namba tisa katika jeshi la Iraq: Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kina nafasi kubwa katika vita vya ukombozi wa Mosul..

Maoni katika picha
Bwana Qassim Jaasim Nizaar kiongozi wa kikosi cha mizinga namba tisa katika jeshi la Iraq wanao shiriki katika oporeshen ya tunakuja ewe nainawa, alipo tembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) leo siku ya Alkhamisi (4 Jamadil Ula 1438h) sawa na (02/02/2017m) alisema kua; Hakika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kina nafasi kubwa katika vita vya ukombozi wa Mosul, na wataendelea kua na umuhimu mkubwa katika hatua zijazo inshallah.

Akabainisha kua: “Hakika kikosi hiki kina uwezo mkubwa wa kupigana na uwepo wao una nafasi kubwa sana hususan katika vita vya kukomba kitongoji cha Bashiir, uzoefu walio pata katika kitongoji hicho umechangia pakubwa katika kutekeleza jukumu la mapambano na mpangilio wa mawasiliano na vikosi vingine katika vita vya kuikomboa Mosul na kuwamaliza kabisa magaidi wa kidaesh.

Mkuu huyu alitembelea pia makao makuu ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, akajadiliana pamoja nao hali ya vita na maendeleo ya mwisho yaliyo patikana katika uwanja wa vita vya kuukomboa mji wa Mosul, akawapa matumaini kikosi cha wapiganaji kinacho undwa na watu wa Mosul kua; wasiwe na wasi wasi tena sasa hivi jeshi lina uwezo mkubwa wa kivita linaweza kuihami Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu.

Tunapenda kusema kua: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilisisitiza Kwamba wataingia katika vita hivi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa hapo nyuma, na kwamba sasa hivi ni wakati wa kushinda, pia walisema kua Tal-afur inahitaji muda kuikomboa lakini hauko mbali, mpango ni mzuri na unaenda kama ulivyo pangwa, tutamshangaza adui kwa ubunifu wa kivita na upiganaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: