Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu akagua maendelea ya mradi wa nyumba za Alkafeel za makazi..

Sehemu ya ziara
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amekagua maendeleo ya mradi wa nyumba za Alkafeel za makazi, ambazo zinajengwa rasmi kwa ajili ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hilo alilifanya katika jaula yake ya kutembelea miradi, alifatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqari (d.t) na jopo la viongozi wa idara tofauti kwa ajili ya kuangalia gazi za mwisho zinazo endelea kufanywa katika mradi huu kutokana na ratiba ya muda ilivyo pangwa, na kuangalia matatizo na vikwazo vinavyo weza kuchelewesha kukamilika kwa mradi.

Katika matembezi haya ya kiongozi wa kisheria pamoja na jopo alilofatana nalo, waliambatana na kiongozi mtendaji wa shirika la Sibtwain ambalo ndio watekelezaji wa mradi Ustadh Maahir Abdul-ameer Salman, aliwatembeza na kuwafafanulia kwa urefu kuhusu kazi zinazo endelea hivi sasa na hatua ambazo zimesha kamilika na ambazo bado hazijakamilika pamoja na zile ambazo ndio zinaanza sasa, kama vile kuweka lami katika njia kubwa na ndogo zilizopo ndani ya mradi huo, pamoja na kazi ya kuweka marumaru katika baadhi za njia na kazi zingine za umaliziaji katika majengo ya shule na nyumba za watumishi.

Kumbuka kua ilitangazwa siku za nyuma kukamilika kwa ujenzi wa nyuma za makazi katika mradi huu (nyumba za Alkafeel za makazi) zipatazo (831), hakika sura ya kazi imeenda vizuri na inatoa picha nzuri ya kukamilisha kazi zilizo baki ambazo nyingi zipo katika hatua za mwisho kabisa za ukamilifu wake, na zinatarajiwa kukamilika muda si mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: