Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika mkutano wa kuandaa kongamano la pili kuhusu Ataba zilizopo katika ulimwengu wa kiislamu..

Sehemu ya mkutano
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika mkutano wa kuandaa kongamano la pili kuhusu Ataba zilizopo katika ulimwengu wa kiislamu linalo lenga kukuza mawasiliano na kusaidiana kati yao, na kua na khutuba za dini za aina moja za msimamo wa kati zitakazo jibu mashambulizi ya matakfiri wanao tishia umma wa kiislamu na kuondoa mmomonyoko wa maadili katika jamii ya kiislamu, mara ya kwanza kongamano kama hili lilifanyika katika haram ya imamu Ridha (a.s) na mara ya pili litafanyika katika Atabatu Husseiniyya tukufu katika mwezi wa Rajabu ujao katika siku za kupewa utume (mab’ath) kwa mtume mtukufu.

Yamejadiliwa mambo mengi katika kikao hiki, miongoni mwa yaliyo jadiliwa ni kuchapishwa kwa kitabu cha pamoja kati ya Ataba zote na Mazaru (maeneo matukufu) yote, kitabu hicho kiandikwe kwa lugha tofauti na kigawiwe kwa watu wanaokuja kufanya ziara kwa mamilioni ya nakala, hapo yalitolewa maoni mengi kuhusu jina la kitabu hicho na maudhui zake kutoka kwa wawakilishi wa Ataba na Mazaru, wakakubaliana kuunda kamati itakayo husika na utunzi wa kitabu hicho, halafu wakajadili kuhusu kanuni za kamati za kudumu na kamati za mpito, na mwisho walichagua maudhui ya (Haki za zaairu na familia na mwanamke) kua zitajadiliwa katika kongamano lijalo.

Kumbuka kua kongamano la kwanza la Ataba tukufu na mazaru matakatifu yaliopo katika ulimwengu wa kiislamu lilifanyika katika mji wa Mash-hadi tukufu (Iran) na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Ataba mbali mbali na Mazaru matukufu, ulisisitizwa umuhimu wa kutambulishwa zaidi utukufu wa malalo matakasifu ya Ahlulbait (a.s), na hivi vikao vya maandalizi vinavyo endelea kufanywa kila baada ya muda fulani ni dalili ya kulipa umuhimu swala hili na kuhakikisha linazaa matunda mazuri yatakayo changia kutolewa huduma nzuri kwa mazuwaru wa maeneo haya matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: