Kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu daktari Haidari Bahadeli amesisitiza kua; mradi wa (matibabu bila malipo) unao lenga wakazi wa mijini na vijijini katika mikoa yote ya Iraq, kupima afya zao na kuwapatia tiba kutokana na matatizo yayo bila malipo yeyote ni endelevu, tutaendelea kuupanua na kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi katika mradi huu ili tuweze kufikia vijiji fakiri na vyenye shida kubwa ya huduma hii kama ilivyo pangwa na idara ya hospitali kuwapatia msaada wa kimatibabu.
Hayo yalisemwa katika ziara ya mwisho iliyo fanyika katika mji wa Rashad mashariki ya mji mkuu wa Bagdad, katika mji huo walipimwa na kutibiwa karibu watu (1,100), huduma walizo pata bure ni, upimaji wa macho na upimaji wa watoto pamoja na kutibiwa bure kwa kila aliye kutwa na tatizo, pamoja na kupima maradhi ya tumbo kwa wakubwa na kupewa dawa kila aliye kutwa na tatizo, hali kadhalika kulikua na wauguzi waliokua wakishughulika na wenye vidonda pamoja na maradhi ya sukari.
Wagonjwa wa mji huu waliishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa juhudi hizi za kibinadamu, huduma hii ina umuhimu mkubwa sana kwao, na imewatosheleza na shida ya kwenda katika vituo vya afya ambavyo pia havina huduma bora ya kiwango cha juu kama iliyo tolewa.