Atabatu Abbaiyya tukufu yaendelea na ziara zake katika vikosi vilivyopo kwenye uwanja wa vita kwa ajili ya kutoa misaada toka kutolewa kwa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu hadi leo, katika ziara hii iliyodumu siku tano tumetembelea vikosi vingi vilivyopo katika miji ya, Tal-abatwa, Talfarisi, na Ainujahashi pamoja na maeneo mengine, ziara hii ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa dini mkuu yanayo wataka watu kuwatembelea wapiganaji watukufu na kuwapa misaada sambamba na kuwapongeza kwa ushindi walio pata kipindi cha mwisho kutokana na ujasiri wao.
Kiongozi wa msafara Shekh Haidari Aaridhiy kutoka katika kitengo cha dini aliiambia Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji waliopo katika mstari wa mbele katika uwanja wa vita toka ilipo tolewa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu hadi leo, ziara hii katika mji wa Mosul ni sehemu ya muendelezo wa ziara kama hizi ambazo zimesha fanywa siku za nyuma, kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), na misaada hii kwa uhakika ni zawadi kutoka katika ofisi ya Marjaa dini mkuu muheshimiwa Sayyid Ally Hussein Sistani (d.dh.w), tumegawa vitu vingi miongoni mwa mahitaji muhimu kwa wapiganaji, mfano: Mavazi ya kujikinga na baridi, kutokana na baridi kali iliyopo katika mji wa Mosul kwa sasa pamoja na aina mbali mbali za vyakula”.
Akaendelea kubainisha kua: “Ziara hii iliyo dumu kwa siku tano imevifikia vikosi mbali mbali vya wapiganaji wa hashdi sha’abi miongoni mwake ni: kikosi cha Sayyid Shuhadaau (a.s) wapiganaji wa Vijana wa mfano, kikosi cha Imamu Ali (a.s) wapiganaji wa imamu Ali (a,s) wapiganaji wa Hizbullah, wapiganaji wa Answaar Marjiiyya, kikosi cha Tufufu, kikosi cha Muntadhir (a.f) waliopo katika msitari wa mbele kwenye miji ya Tal-abatwa, Talzalatwa, Talfarisi na Tilalbaaj, Ainujahashi na kijiji cha Saadiyya, wapiganaji walitupokea kwa bashasha kubwa wakatusisitizia kua wako imara na wataendelea kubaki katika uwanja wa vita hadi waigomboe shibri (sehemu) ya mwisho kabisa katika aridhi tukufu ya Iraq”.
Akaendelea kusema kua: “ Hakika wairaq kama uwajuavyo wako imara na wataendelea kupambana hadi tone la mwisha la damu yao kwa ajili ya kuilinda aridhi ya Iraq na watu wake pamoja na maeneo matakatufu, hakika kila ziara hua tunawakuta wapiganaji wakiwa katika kiwango cha juu kabisa cha ujasiri na kujiamini hili sio jambo geni kwao, mtu anae acha mali na familia yake, akaja katika eneo hili kwa ajili ya kupambana na magaidi na kuwatoa katika aridhi ya Iraq lazima awe jasiri, shujaa na mwenye kujiamini”.
Tunapenda kusema kua; Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji vilivyopo katika uwanja wa vita na kutoa misaada kwa wapiganaji wetu watukufu toka kutolewa kwa fatwa hadi leo kwa ajili ya kuhakikisha muendelezo wa mapambano dhidi ya magaidi wa kidaesh.