Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kikao rasmi na ugeni wa wataalamu wa kiiraq kwa ajili ya maandalizi ya maonyesho yao yatakayo fanyika mwezi wa nne ujao..

Maoni katika picha
Katika kuheshimu uwezo na vipawa vya wairaq na kuwachukulia kua ni tunu za taifa zinazo tafsiri fikra za wairaq, na kutokana na usimamizi unaofanywa na viongozi wakuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) baada ya adhuhuri ya leo Juma Mosi (6 Jamadil Ula 1438h) sawa na (04/02/2017m) kimefanyika kikao cha tatu kati ya wataalamu wa kiiraq na viongozi wakuu wa Ataba tukufu.

Kikao hiki ni kwa ajili ya kutangaza muda rasmi utakao fanyika maonyesho ya wataalamu na wabunifu na kukamilisha mahitaji ya maonyesho hayo, yanatarajiwa kua ya siku tatu kuanzia tarehe (5-7) ya mwezi wa nne katika jengo la shekh Kuleini (q.s) lililopo barabara ya (Bagdad/Karbala), zitatolewa tafiti za masomo pamoja na maonyesho ya ubunifu wao katika fani za tiba, uhandisi, sayansi, kilimo, polisi na jeshi pamoja na mengineo.

Kiongozi wa maonyesho Ustadh Leeth Allaaq aliiambia Alkafeel kua: “Maandalizi ya maonyesho haya yamekua ya aina yake kwa sababu yatasimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na yatahusisha nyanja mbali mbali za kiufundi na kitaalamu, tayali imesha wekwa mipango na taratibu za kiidara pamoja na kuanza kutolewa mialiko na mambo mengine, hakika kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ametupa msaada mkubwa ambao hatujaupata kwa mtu mwingine yeyote, ameonyesha kuguswa na swala hili na kutupatia kila tulicho hitaji kwa ajili ya kuwahudumia wataalamu na wabunifu wa kiiraq”.

Akaendelea kusema kua: “Tumeichagua Atabatu Abbasiyya tukufu kwa sababu ni sehemu muwafaka kutokana na utukufu wake, kwani sisi tulikua tunahitaji kupata sehemu takatifu ya kushirikiana nayo, unapo fanya kazi na watu watukufu mtashirikiana kwa uwazi na uaminifu”.

Akaongeza kua: “Maonyesho haya yatamuhusisha mtu yeyote mwenye ubunifu wa aina yeyote na yanalenga kulea vipaji vya wairaq, na kwa namna ya pekee tunatoa shukrani za dhati kwa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kupokea fikra za wataalamu na ubunifu wao”.

Tunapenda kusema kua; maonyesho yatakayo fanyika, yanatokana na msimamo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kujali na kuwapa umuhimu wataalamu na wabunifu wa kiiraq na kutaka kuingiza ubunifu wao katika utendaji halisi, ugeni wa wataalamu na wabunifu wa kiiraq waliitembelea Ataba tukufu siku za nyuma kwa ajili ya kuangalia miradi yake na mafanikio iliyo nayo ili kufungua milango ya ushirikiano baina yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: