Atabatu Husseiniyya tukufu yafanya hafla ya kukumbuka kifo cha kiongozi wa mimbari ya Husseiniyya Shekh Dkt Ahmadi Waailiy (t.th)..

Maoni katika picha
Atabatu Husseiniyya tukufu alasiri ya siku ya Juma Mosi (6 Jamadil Ula 1438h) sawa na (04/02/2017m) ilifanya hafla ya kukumbuka athari na mafanikio makubwa aliyo pata Shekh Dkt Waailiy (r.a) katika kuitumikia mimbari ya husseiniyya, hafla ilifanyika katika ukumbi wa Khatamul Anbiyaa (s.a.w.w), Dkt Waailiy alitumia umri wake katika uelimisha vizazi misingi ya uislamu halisi kwa kutumia hekima na mawaidha mema, hafla ilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu husseiniyya pamoja na sehemu kubwa ya wanazuoni, mashekh na makhatibu wa mimbari husseiniyya, ilifunguliwa kwa kusomwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kumrehemu Shekh na mashahidi wa Iraq wote, kisha alizungumza kiongozi wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu muheshimiwa shekh Abdulmahadi Karbalai (d.i) miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo tunamkumbuka mtu mtukufu aliye kua na nafasi kubwa katika kuitumikia mimbari ya husseiniyya, mimbari ambayo ni msingi muhimu katika kuhifadhi dini ya uislamu na kutoa mafundisho ya Ahlulbait (a.s), kujitolea kwa wapiganaji tunako shuhudia katika uwanja wa vita ni zao la mimbari hii tukufu iliyo hudumiwa na marehemu shekh Waailiy (t.th), huyu ni mtu mtukufu ambaye huchukuliwa kua ni kiongozi wa mimbari ya husseiniyya na ni haki yake kwetu kudumisha kumbukumbu zake na mwenendo wake mtukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Kuna haja ya kuisoma madrasa ya Ahlulbait (a.s) kwa undani, madrasa hii tukufu iliyo watoa makhatibu wakubwa kama shekh Waailiy, tunatarajia kwa walimu wetu na ndugu zetu watukufu watukusanyie mazuri aliyofanya katika uhai wake katika kitabu na kukipa jina la (Khaswaaisu Waailiy)”.

Kisha baada yake aliongea mtumishi wa mimbari husseiniyya Shekh Muhammad Baaqir Muqadasiy miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika tukiangalia athari ya mimbari husseiniyya katika jamii tunaiona katika mambo mengi, miongoni mwake tunaona wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaishi katika maadili mema, na mimbari ndio inayojenga tamaduni na maadili mazuri kwa waumini, shekh Waailiy (r.a) alikua ni kiongozi wa mimbari ya husseiniyya alifanikisha kuleta njia mpya za uwasilishaji wa mihadhara, tunaweza kusema alikua mtu wa kwanza aliye tumia njia ya tafsiri maudhui katika aya za Qur’an tukufu, alikua mtu mahiri sana aliye kusanya elimu ya kisekula na kihauza jambo hili lilichangia sana kuleta athari katika mimbari”.

Halafu ikasomwa qaswida ya kimashairi iliyo zungumzia utukufu wa mimbari ya husseiniyya, baada ya qaswida hiyo akazungumza shekh Ibrahim Nasraawi ambaye alisema kua: “Hakika dokta Waailiy (t.th) alikua mtu wa pekee, alijulikana na kila mtu aliye hudhuria majlisi zake, alikua na athari kubwa katika kutumikia mimbari ya husseiniyya, kila mtu anafahamu athari kubwa aliyo kua nayo katika ufikishaji wa ujumbe, aliweza kutambulisha tamaduni za kiislamu kwa uwazi kabisa katika njia nzuri inayo kubalika kwa wote wanao msikiliza”.

Kisha ikaonyeshwa filamu yenye anuani isemayo (Swadal Khuluud) inayo elezea uhai wa dokta Waailiy (r.a) na mwenendo wake katika kutumikia mimbari ya husseiniyya, hafla ilikhitimiswa kwa kupewa zawadi mjukuu wa marehemu shekh aliye wakilisha familia yake ambapo alipewa midani yenye picha ya mimbari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: