Kuhuisha kumbu kumbu ya shahada ya bibi Zaharaa (a.s) kitengo cha Sha’airi na Mawaakibu Husseiniyya chaanza msimu wa huzuni za Fatwimiyya awamu ya tisa..

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kitengo cha Sha’airi na Mawaakibu Husseiniyya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu jana siku ya Juma Mosi (6 Jamadil Ula 1438h) sawa na (04/02/2017m) wamefungua msimu wa huzuni katika eneo la baina ya haram mbili tukufu kwa kufanya kumbu kumbu ya awamu ya tisa ya shahada ya mtakasifu mbora wa wanawake wa duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na itaendelea kwa siku kumi.

Hafla ilipata muitikio mkubwa kwa viongozi wa Ataba tukufu na kundi kubwa la watu waliokuja kufanya ziara, ilifunguliwa kwa kusoma Qur’an tukufu kisha ikafatiwa na muhadhara uliotolewa na shekh Aamir Karbalaai kutoka katika kitengo cha dini ndani ya Ataba tukufu, alielezea kwa ufupi kuhusu uhai wa bibi zaharaa (a.s) na masaaib aliyo pata baada ya kufariki kwa baba yake (s.a.w.w), kisha alipanda mimbari msomaji wa mashairi ya husseiniyya; akasoma mashairi ya husseiniyya yaliyo leta huzuni na kujenga taswira ya msiba wa bibi Zaharaa (a.s), pia kulikua na picha za Huru zilizo chorwa na wanafunzi wa shule za Ameed katika mbao ambazo pia zilijenga huzuni hasa kwa watoto na kujenga taswira ya msiba wa bibi Zaharaa (a.s).

Makamo rais wa kitengo cha Sha’airi na Mawaakibu Husseiniyya ustadhi Maazin Wazaniy aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na maelekezo ya viongozi wa kisheria katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kitengo cha Sha’airi na Mawaakibu kimerejea kufanya kumbu kumbu zote za minasaba ya Ahlulbait (a.s) iliyo kua inafanywa katika miaka ya nyuma, na amabayo utawala uliopita (wa Sadam) uliipiga marufuku, miongoni mwa minasaba hiyo ni huu wa huzuni za Fatwimiyya (kukumbuka kifo cha bibi Fatuma (a.s)) unaofanywa kila mwaka katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu ambayo jana umefanyika ufunguzi wa maonyesho yake rasmi, maonyesho ambayo hutoa mafunzo na picha halisi ya maisha ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa kutumia michoro, sauti, vitabu na khutuba zake ikiwa pamoja na mafunzo ya hadithi Kisaa, Mubahala na mengineyo, maonyesho haya hayakuwepo zamani, ni miongoni mwa vitu vipya vilivyo ongezwa na kitengo hiki kwa kushirikiana na vitengo vingine katika Ataba tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Katika muda wa siku kumi mfululizo zitafanyika majlisi za huzuni ndani ya malalo mawili matukufu na katika eneo la katikati ya haram mbili, hali kadhalika kutakua na maukibu ya pamoja ya watu wa Karbala ambayo itafanya matembezi siku ya (14 Jamadil Ula) na kutakua na maukibu nyingine ya wanawake itakayo huisha dhulma aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s) pia zitashiriki maukibu zingine nyingi kutoka maeneo tofauti”.

Tunapenda kukumbusha kua; kitengo cha Sha’airi na Mawaakibu Husseiniyya katika kila mwaka hua kinafanya kumbukumbu za huzuni za Fatwimiyya (kukumbuka kifo cha bibi Fatuma a.s) katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu kwa muda wa siku kumi, hufanyika mambo mengi ya kuhuisha huzuni kuanzia maonyesho (Panorama) pamoja na majaalisi za huzuni na hushiriki Mawaakibu tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: