Katika ziara za makazi yake: kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji..

Maoni katika picha
Kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na katibu mkuu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na jopo la viongozi wengine, jana siku ya Juma Mosi (6 Jamadil Ula 1438h) walifanya ziara katika makao makuu ya viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji yaliyopo katika jengo la Alqami lililo chini ya Ataba tukufu katika barabara ya (Baabil - Karbala) kwa ajili ya kukagua utendaji wao na mafanikio waliyo pata pamoja na kujipanga kwao kwa vita zijazo, walipokelewa na kiongozi mkuu ustadh Maitham Zaidiy pamoja na jopo la wapiganaji wa kujitolea.

Baada ya kupokea maelezo mazuri kutoka kwa wapiganaji, muheshimiwa alionyesha umuhimu wa kuwepo kwa mipango madhubuti itakayo saidia kufikiwa malengo kwa hasara ndogo na umuhimu wa kudumisha mawasiliano baina yao na viongozi wa kijeshi na vikosi vingine vya hashdi sha’abi, pia alisisitiza uvaaji wa ngao na kofia ngumu wakati wa mapambano kwani Ataba tukufu katika siku za nyuma iliandaa ngao elufu moja na kofia ngumu.

Tunapenda kukumbusha kua; Atabatu Abbasiyya tukufu ndio mfadhili mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika nyanja zote, kama ilivyo tangaza na kubainisha kua: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ndio muwakilishi wao pekee katika kuitikia fatwa tukufu ya kuilinda aridhi ya Iraq na maeneo matukufu iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: