Idara ya makuzi ya watoto iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka hema rasmi kwa ajili ya mafunzo ya skauti (Scout) kwa wanafunzi wa upili (sekondari) wa shule ya Sayyid Almaau ambayo ni miongoni mwa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s), hema limewekwa katika jengo la Shekh Kuleini (q.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika barabara (Bagdad – Karbalaa) na lilidumu kwa muda wa siku tatu, hii ni miongoni mwa ratiba ya uwekaji wa maheka ya skaut (Scout) yatakayo husisha wanafunzi wa umri tofauti kwa lengo la kukuza vipaji vya wanafunzi kimuili na kifikra na kunufaika na vipawa vyao.
Mwalimu wa ratiba hii ustadh Ali Hussein Abduzaidi aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kama mnavyo fahamu kua idara yetu imeanza kuweka mahema ya scout kwa wanafunzi wa umri tofauti katika vipindi vya likizo, kwa ajili ya kunufaika na kipindi hiki na kutumia muda ambao mwanafunzi angekaa bila shughuli, tumeanza kwa kuweka hema ambalo tumelipa jina la (Jabali ya subira) kwa ajili ya shughuli rasmi za scout, hema hili tumeliweka katika jengo la shekh Kuleini (q.s) na wameshiriki wanafunzi wa upili (sekondari) sitini (60) wa shule ya Sayyid Almaau ambayo ni miongoni mwa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaendelea kusema kua: “Shughuli hizi zimedumu kwa muda wa siku tatu zinalenga kukuza vipaji vya wanafunzi kimuili (kimazoezi) na kifikra na kugundua vipaji vya wanafunzi katika usomaji wa Qur’an, uchoraji, uigizaji, hati na vinginevyo, tumeweka ratiba ambayo imehusisha vitu vyote kwa ajili ya kugundua vipaji vya wanafunzi ikiwa ni pamoja na ratiba ya utoaji wa mihadhara pamoja na utoaji wa huduma ya kwanza kwa kushirikiana na kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu, na upande wa ratiba ya utoaji wa mihadhara ya kidini tumewahusisha kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kusema kua: “Mwisho wa zoezi hili tutafanya kongamano dogo la kuonyesha vipaji vitakavyo gunduliwa, ambalo litapambwa na vitu vingi miongoni mwake ni kikosi cha qaswida na maigizo ikiwa ni pamoja na maonyesho ya fani za kupigana na litahudhuriwa na baadhi ya walimu kutoka katika kitengo cha malezi na elimu ya juu”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu huendesha na husimamia ratiba nyingi za maswala ya kimasomo na kitamaduni ndani na nje ya Ataba tukufu na miongoni mwa ratiba hizo ni kuendesha mafunzo ya scout kwa wanafunzi ambayo yanamchango mkubwa sana katika kuweka misingi imara ya mafundisho ya dini tukufu ya kiislamu na mwenendo wa Ahlulbat (a.s) na kuwafanya waipende nchi yao na raia wake na kuingiza katika mwenendo wa maisha yao ya kawaida ya kila siku.