Atabatu Abbasiyya tukufu yahuisha kumbukumbu ya mazazi ya bibi Zainabu (a.s) katika jiji la London kupitia tawi lake la Maahadi ya Qur’an tukufu katika jiji hilo..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa kwa ajili ya mnasaba wa kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s) kupitia tawi lake la Maahadi ya Qur’an tukufu lililo chini ya kitengo cha maafira ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na ustadh Mustwafa Ally kisha uliwasilishwa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliosomwa na mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an na kuifasiri na kuichapisha shekh Dhiyaau-dini Zubaidiy ambaye alizungumzia baadhi ya matukufu ya bibi Zainabu (a.s) na akafahamisha kuhusu mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu hususan mafanikio ya Maahadi ya Qur’an pia akatoa shukrani kwa wahudhuriaji na kuwafikishia salamu kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i).

Halafu akazungumza Aayatullahi Sayyid Faadhil Milaani(d.b), ambaye alianza kwa kusifu mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na akazungumzia baadhi ya misimamo muhimu aliyo kua nayo bibi Zainabu (a.s) katika kulinda mwenendo wa kizazi kitoharifu wakati wa uhai wake.

Kisha ulifatia ujumbe wa Maahadi ya Qur’an tukufu katika jiji la London ulio wasilishwa na ustadh Sayyid Haidari Mussawiy mmoja wa wajumbe wa Maahadi hiyo, ambaye aliwasifu watumishi wa Maahadi na wasimamizi wa hafla hii katika mnasaba huu muhimu. Kiongozi wa Maahadi ya Qur’an katika jiji la Londan akafurahisha hafla kwa kusoma mashairi mazuri ya kumsifu bibi Zainabu (a.s).

Halafu vyeti vikagawiwa kwa wahitimu wa kozi mbali mbali zilizo tolewa na Maahadi na zikatolewa zawadi kwa wahudhuriaji wote za tabaruku kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ilikua na mahudhurio mazuri ikiwa ni pamoja na kupata bahati ya ushiriki wa Aayatullahi Milaani na muwakilishi wa Marjaa mkuu katika mji wa London Alama Sayyid Said Khalkhaali pamoja na balozi wa Iraq wa Wingereza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: