Hospitali ya rufaa Alkafeel yatangaza nafasi za kazi..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza nafasi za kati kwa sharti muombaji awe ni raia wa Iraq na akamilishe vigezo vya nafasi anayo omba.

Wanao hitajika ni:

Kwanza: Kiongozi wa kitengo cha tiba, awe na sifa zifuataza;

  • - Awe na kadi ya utumishi wa tiba katika moja ya fani za udaktari na Diploma ya General Medicine.
  • - Awe ana Masta ya uongozi wa hospitali (Hospital Administration).
  • - Awe na uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa idara ya tiba.
  • - Awe anafahamu lugha ya kiengereza (kusoma na kuandika).

Pili: Kiongozi wa kitengo cha uuguzi, anatakiwa awe na sifa zifuatazo:

  • - Awe na shahada kutoka katika chuo cha uuguzi.
  • - Awe na Masta ya ungozi wa uuguzi katika idara za hospitali.
  • - Awe na uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa wauguzi.
  • - Awe anafahamu lugha la kiarabu na kiengereza (kusoma na kuandika).

Uongozi wa hospitali unawataka wenye sifa hizo waende katika jengo la hospitali huko Karabala njia ya Najafu Alhauli/ barabara ya Hamza mdogo wakiwa na vielelezo vyao, au wapige simu namba: (07602329999) au (07602344444).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: