Shindano litahusisha mada zifuatazo:
- Maarifa ya Qur’an na tafsiri yake na mienendo za tafsiri pamoja na visomo vya Qur’an na mambo mengine yanayo husu Qur’an tukufu.
- Mada za kiakili na kiitikadi zitahusisha mambo tofauti ya kifikra, itikadi na falsafa za watu wa Basra.
- Mada za Fiqhi, Usulu, Diraya na hadithi.
- Mada za lugha, zitahusisha Nahau, Swarafu, Sauti, Balagha na mengineyo katika mambo yanayo husu maendeleo ya lugha na mchango wa watu wa Basra katika hilo.
- Mada za ushairi, zitahusisha aina tofauti za mashairi na mchango wa wanamashairi wa Basra ikiwa ni pamoja na mashairi ya Husseiniyya na Ahlulbait (a.s) kwa ujumla.
- Mada za kihistoria, zitahusisha historia ya mji wa Basra katika zama tofauti: kabla ya uislamu, wakati wa uislamu, zama za utawala wa Umawiyya, utawala wa Abbasiyya, tawala zingine, utawala wa Othmaniyya na hali ya zama hizi.
- Mada kuhusu maeneo matukufu na makaburi ya waja wema yaliyopo katika mji wa Basra (maelezo ya kina).
- Mada kuhusu elimu za watu wa Basra na mchango wao katika uwanja wa elimu tofauti.
- Historia kuhusu ujenzi wa mji wa Basra na mustakabali wake.
- Kuhakiki bitabu kale.
- Uhakiki yakinifu katika vitabu vilivyo andikwa kuhusu mji wa Basra katika nyanja tofauti.
- Mtazamo wa wanahabari kuhusu watu wa Basra.
- Siasa za watawala kuhusu watu wa Basra na athari ya siasa hizo katika ujenzi wa mji kifikra, kimajengo na kitamaduni na vinginevyo.
- Mada kuhusu athari na utalii.
- Mada kuhusu Jografia ya Basra ya zamani na ya sasa.
- Mada kuhusu uchumi wa Basra.
Zimeandaliwa zawadi kwa washindi kumi wa kwanza kama ifuatavyo:
- Zawadi ya kwanza: milioni tano dinari.
- Zawadi ya pili: milioni nne dinari.
- Zawadi ya tatu: milioni tatu dinari.
- Zawadi ya nne: milioni moja dinari.
- Zawadi ya tano: milioni moja dinari.
- Zawadi ya sita: milioni moja dinari.
- Zawadi ya saba: milioni moja dinari.
- Zawadi ya nane: milioni moja dinari.
- Zawadi ya tisa: milioni moja dinari.
- Zawadi ya kumi: milioni moja dinari.
Kutakua na zawadi zitakazo gawiwa kwa washiriki wengine pia, kumbuka kua mwisho wa kupokea tafiti (vitavu) vya washiriki ni (01/10/2017m) kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu katika namba zifuatazo: (07709050191 – 07604287317) au unaweza kuandika barua pepe kwa anuani ifuatayo: (basrah@alkafeel.net) au unaweza kutembelea ofisi zetu zilizopo: (Basra - barabara – Bagdad – mtaa Alghadeer – mkabala na mahakama kuu).