Daru Rasuli A’adhamu (s.a.w.w) iliyopo katika kituo cha Ameed duwaliyyu lilbuhuuthi wa dirasaati kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha kwanza cha sira ya mtume (s.a.w.w) kilicho pewa jina la (Sira ya mtume katika riwaya za imamu Swadiq (a.s)) kilicho andikwa na dokta Juma Hamdani, ambaye alisema kua:
“Umuhimu wa kitabu hiki, masomo ya yaliyo andikwa ndani yake ni miongoni mwa mambo nyeti sana, kwa sababu ni sira ya mbora wa viumbe katika uso wa aridhi, pamoja na kwanba ndio mwanzo wa kuandikwa kwa historia ya waarabu na waislamu, pia kuna sababu nyingi zilizo pelekea kuandika sira ya mtume kwa riwaya za imamu Swadiq (a.s) kwa kua ni mtu mwenye hadhi kubwa kihistoria, ikiwa ni pamoja na ukweli kua riwaya zake (a.s) zinafasiri Qur’an na sunna za mtume (s.a.w.w), tunapo soma sira ya mtume tukufu inaoana na mwenendo wake (s.a.w.w) pamoja na misimamo yake, dalili inapotoka kwa imamu Swadiq (a.s) inakua imetoka katika akili, fikra na mantiki salama”.
Dokta Aadil Nadheer Biri ambaye ni rais wa Daru Rasuli (s.a.w.w) alisema kua: “ Hakika lengo la Daru Rasuli ni kulinda sira ya mtume mtukufu na kuitakasa kutokana na uharibifu na kuiweka katika sura nzuri hiki ndio kipawa mbele chetu, bali ndio lengo kuu ambalo imeanzishwa hii Daru Rasuli kwa ajili yake”.
Akaendelea kusema kua: “Bila shaka riwaya za Ahlulbaiti (a.s) ndio za kweli kabisa kuhusu maisha ya mtume (s.a.w.w) kwa hiyo kuandika kitabu cha sira kwa kutegemea riwaya kutoka kwa mmoja wa maimamu watakasifu (a.s) ni jambo muhimu katika kufikia malengo yetu, tumechagua kutumia njia hii katika uandishi wa vitabu hivi, lengo letu kuu ni kufundisha tamaduni za mtume (s.a.w.w) na Aali zake watoharifu (a.s) mafundisho ambayo yanaitosheleza jamii katika kila kitu, na kuthabitisha uwelewa sahihi na kufuata mwenendo bora kwa kila muislamu”.
Tunapenda kukumbusha lengo la kuanzishwa kwa Daru Rasuli A’adhamu (s.a.w.w) ni kujaribu kuoanisha mitazamo baina ya madhehebu za kiislamu, katika kufanyia kazi khutuba za mtume ili zitusaidie kupata umoja katika khutuba za kidini na kusahihisha mitazamo kinzani kati yetu, na kufaidika kutokana na turathi za mtume (s.a.w.w) katika maswala ya kielimu, bila kusahau elimu na falsafa ya mtume ni salama zaidi.