Idara ya makuzi ya watoto iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa makumi ya machapisho ya visa sambamba na jarida la Riyaahaini ili kulifanya likae mikononi mwa watoto (lipendwe na watoto), visa hivyo vimeandikwa katika vijitabu vidogo vidogo vyenye randi inayo vutia kwa watoto, kila kijitabu kinakua na visa vilivyo pambwa kwa picha vinazo changia katika kuamsha kipawa cha mtoto na kumfanya akue katika mwenendo wa itikadi sahihi ya kiislamu.
Rais wa wahariri wa jarida hili, Ustadhi Ally Badri aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inalipa kundi la watoto umuhimu mkubwa sana kwa sababu wao ndio viongozi wa nchi wa baadae, na kujenga jamii kunaanzia katika kujenga watoto, kwani wana uwezo mkubwa wa kusoma na kubadilika, baada ya kutoa jarida la Riyaahaini tuliona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa chapisho lingine litakalo enda pamoja na jarida na lenye vionjo vizuri kwa watoto, ndio tukaamua kutoa machapisho ya visa katika vijitabu vidogo vidogo vyenye rangi za kuvutia kwa watoto na vinavyo changia pakubwa katika kuamsha uwezo wa watoto kwa njia sahihi”.
Akaendelea kusema kua: “Machapisho haya yamekusanya visa vya Qur’an tukufu, pamoja na picha zenye anuani isemayo maarifa ya Qur’an navyo ni miongoni mwa vitabu bora zaidi vinavyo zungumza kuhusu Qur’an tukufu, vijitabu hivi vinakua vimeandikwa aya fupi fupi kwa rangi zinazo pendwa na watoto, kwa namna ambayo mtoto anaweza kuzihifadhi kwa wepesi, kwa mfano mada ya Israfu katika aya ya Qur’an: (Kuleni na kunyweni wala msifanye isirafu) pamoja na sherehe fupi na hadithi ya mtume mtukufu kutoka kwa Ahlulbait (a.s) na zinakua zimepambwa kwa rangi nzuri zinazo saidia akili ya mtoto kuhifadhi, ndani ya kijitabu kimoja kitamsaidia kufahamu mambo mengi kuhusu Qur’an tukufu”.
Akaendelea kubainisha kua: “Vijitabu hivi vinahusisha kijibabu maalumu kinacho elezea watu wa nyumba ya mtume (s.a), kinaandika maelezo kuhusu kila imamu maasumu (mtakasifu) (a.s), kijitabu cha kwanza kimemzungumzia mtume Muhammad (s.a.w.w) na cha pili kimemzungumzia imamu Ali (a.s) kisha kikamzungumzia bibi Zaharaa (a.s) kisha vinaendelea kuzungumzia maimamu wengine wote (a.s) kila chapisho linaandika kuhusu imamu kwa ufupi kutokana na uwezo wa akili ya mtoto, pamoja na kuonyesha ubinadamu wa maimamu (a.s) na kubainisha mazuri katika maneno yao, pia kuna mtiririko wa maelezo kuhusu hashdi sha’abi, ambapo ni visa vya ukweli kuhusu ujasiri wa wapiganaji wa hashdi sha’abi, kwa ajili ya kuwajengea watoto utamaduni wa kujilinda na kuilinda nchi yao, na hutajwa mafanikio yaliyo patikana katika uwanja wa vita, hili linafanywa kutokana na wito wa Marjaa dini mkuu wa kutaka kuwafahamisha watoto ujasiri na mafanikio yanayo patikana katika uwanja wa vita kwa sababu watoto hawafatilii habari”.
Akaendelea kusema kua: “Kuna visa tofauti tofauti katika makumi ya vijitabu vinavyo zungumzia tabia njema na baadhi ya mambo ya kimaadili yanayo jenga makuzi salama ya watoto, pamoja na mtiririko mwingine unao zungumzia watu muhimu huku mtiririko mwingine ukisheheni qaswida na mashairi kuhusu mapenzi ya Ahlulbait (a.s), kila kitabu kina karibia kurasa ishirini, na husambazwa kupitia vituo vya mauzo ya moja kwa moja vya Ataba tukufu au kwa kuvigawa katika shule kwa malipo kidodo”.
Kumbuka kua idara ya watoto ina machapisho mengi yanayo lenga umri tofauti wa watoto kwa ajili ya kujenga kizazi salama chenye kufuata mwenendo na tamaduni za Ahlulbait (a.s).