Mazoezi hai ya vitendo: kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu chakhitimisha kozi ya afya na usalama kazini..

Picha za kukhitimisha kozi
Kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chama cha mwezi mwekundu cha Iraq wamekamilisha kozi ya afya na usalama kazini, katika shughuli za kumaliza kozi hii yalifanywa maonyesho yaliyo lenga kujenga utamaduni wa kulinda afya na kuhakikisha mazingira salama sehemu ya kazi katika vitengo vyote vya Ataba tukufu, na kuongeza maarifa kwa waliopata kozi ya uokozi katika hatua za kwanza.

Washiriki wa kozi walikua ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukutu pamoja na walinzi wa mji (wanajeshi) na watu wa mwezi mwekundu na ilihusu usalama kazini, pia ilihusisha mbinu za kupambana na moto tatiza la kuvunjika kiungo pamoja na namna ya kuamiliana na mtu aliye zimia na majeruhi katika vita na katika maisha ya kawaida, hali kadhalika walifundishwa namna ya kumtoa majeruhi ndani ya uwanja wa vita kwa kutumia njia ambazo zinamlinda muokoaji na hatari ya kushambuliwa kwa kiasi kikubwa, vile vile wamefundishwa namna ya kuendesha gari la wagonjwa katikati ya milio ya risasi.

Mwishoni mwa kozi walifanya mazoezi halisi kwa kushirikiana na chama cha mwezi mwekundu cha Iraq kwa ajili ya kufanyia kazi mambo waliyo soma katika kozi.

Mkufunzi bwana Ally Auda ambaye pia ni kiongozi wa idara ya uokozi alisema kua: “Lengo la kufanya maonyesho hai (halisi) ni kufasiri nadharia walizo soma darasani na kuziingiza katika vitendo halisi, pia ni nafasi ya kila mshiriki kupata uzoefu utakao msaidia siku yeyote atakapo kutana na tukio halisi, tumejitahidi kutengeneza mazingira yanayo fanana na uhalisia kwa ajili ya kuwafanya washiriki wapate mazingatio katika namna bora zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: