Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu akagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Maqaamu imamu Mahadi (a.f) na asifia maendeleo yaliyo fikiwa..

Sehemu ya ziara
Miongoni mwa jaula na ziara anazo fanya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) ametembelea mradi wa upanuzi wa maqaamu imamu Mahadi (a.f) ambao ujenzi wake unaendelea kwa vizuri na kwa haraka, kwa ajili ya kuukamilisha ndani ya muda uliopangwa na katika ubora unao hitajika kama ulivyo sanifiwa.

Rais msaidizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Naswifu aliye fatana na ugeni huo alisema kua: “Kazi za mradi wa upanuzi wa Maqaamu imamu Mahadi (a.f) inaendelea vizuri, baada ya kumaliza hatua ya kwanza na kuingia hatua ya pili, ziara hii ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kukagua maendeleo ya ujenzi na hatua zilizo kamilika inatia msisitizo kwa mafundi kuongeza juhudi ya kazi na kuhakikisha maradi unakamilika kwa wakati ulio pangwa”.

Kumbuka kua mradi wa upanuzi wa maqaamu ya imamu Mahadi (a.f) hatua ya kwanza ilihusisha ujenzi wa ukumbi wa wanawake wenye ukubwa wa mita za mraba (490) na sehemu ya pili inahusisha ukumbi wa wanaume wenye ukubwa wa mita za mraba (310) na sehemu ya watumishi yenye ukubwa wa mita za mraba (150) sehemu iliyo bakia ni ile ya vyoo ambayo inaendelea kujengwa hivi sasa, Atabatu Abbasiyya tukufu ndio wanaofanya ujenzi huu kwa kukarabati jengo lililo kuwepo na kulifanyia upanuzi kwa kuanzia katika kubba hadi kumbi za haram na vyoo, kwa kua sehemu ilipo hii maqaamu (jengo) hauwezi kulifanyia upanuzi katika pande zake tatu, ililazimika upanuzi huu ufanywe upande wa mto Husseiniyya ambao ni upande wake wa magharibi, kwa kiasi cha mita za mraba (1200) na unafika katika maqaamu kwa kutumia milango maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: