Wingu la huzuni za Fatwimiyya latanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu na penbezoni mwake..

Maoni katika picha
Uhuishaji wa kumbukumbu ya kufariki kwa bibi Fatuma (a.s) bibi wa wanawake wa duniani, kumeweka wingu la huzuni za Fatwimiyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu na pembezoni mwake, yamewekwa mapambo meusi kama ishara ya huzuni hii kubwa, na zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu na yamewekwa mabango katika milango na sehemu mbalimbali yanayo onyesha kudhulumiwa kwake (a.s) na yaliyo jiri miongoni mwa misiba na matatizo, haya yote kwa ajili ya kuadhimisha msiba huu na kumliwaza mtume na Aali zake (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu (kama kawaida yake) iliandaa ratiba ya taaziya iliyo husisha mambo mengi, ikiwemo kutolewa kwa mihadhara ya kidini na kufanywa kwa majaalisi maalumu za azaa, pamoja na hayo ilijipanga kupokea mawaakibu (makundi) ya azaa ndani na nje ya mji wa Karbala tukufu, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa maukibu ya pamoja kati ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya siku ya mwezi kumi na nne Jamadil Ula kama sehemu ya kumhani imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tunapenda kusema kua; Mwenyezi Mungu mtukufu ameficha siku ya lailatul qadri ndani ya siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhani mtukufu na akaficha swalatul ustwa (katikati) katika swala zingine alipo sema: (Hifadhini swala na swala ya katikati na msimame kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu), ili mja afanye ibada zaidi ya usiku mmoja katika kuitafuta lailatul qadri, na ili mja aswali sala zote kwa unyenyekevu katika kuitafuta swala ya katikati, tunaweza kusema pia Mwenyezi Mungu mtukufu kwa hekima zake amependa bibi Fatuma (a.s) awe na zaidi ya siku moja ya kukumbuka kufariki kwake (a.s) kutokana na kutofautiana kwa riwaya zinazo taja tarehe ya kufariki kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: