Maahadi ya turathi za mitume (a.s) yaendelea na vikao vya kujadili hali ya elimu na malezi katika nchi..

Maoni katika picha
Baada ya adhuhuri ya siku ya Ijumaa (12 Jamadil Ula 1438h) sawa na (10/02/2017) kilifanyika moja ya kikao miongoni mwa vikao vinavyo endeshwa na Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (masafa) iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Walezi.. baina ya matatizo ya sasa na matarajio ya baadae) ambapo ilijadiliwa hali ya masomo ya malezi katika taifa, na kuangalia namna ya kuboresha mazingira katika swala hilo, walialikwa walimu wa malezi (50) kutoka katika shule za Bagdadi.

Hafla ilifanyika katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s), ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur’an tukufu, kisha Shekh Hussein Turabi ambaye ni kiongozi mkuu wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (masafa) aliongea, miongoni mwa maonezi yake ni: “Msingi wa kazi ni elimu na malezi”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika msingi wa umoja ni neno hilo (elimu na malezi) ambalo lina maana nyingi lakini zote zinalenga kitu kimoja, na zinawaunganisha wana nchi katika jambo la elimu, tukiweza kujenga jamii yenye malezi bora na elimu kuanzia hatua za mwanzo, tutakua tumejenga kizazi chenye kujitambua na chenye uwezo wa kushinda changamoto zinazo kikabili”.

Sekhe Turabi aliendelea kuelezea baadhi ya mambo ya kisheria yanayo husu taasisi za kielimu na kimalezi na namna ya kunufaika na kanuni hizo.

Baada yake kikao kiliendelea na majadiliano, ambapo aliongea mkuu wa kitengo cha malezi ustadh Swabahu Jaasim Muhammad, alisema kua: “Hakika nafasi ya malezi ndio msingi wa kujenga tabia nzuri, hakuna elimu bila ya malezi bora, watu wa malezi pengine wanaweza kughafirika katika kufahamu ukweli huu, na wengine wanaweza kudhani kua elimu ni kusoma vitabu na kufuata selebasi ya masomo, hilo ni kosa ambalo linaweza kutufanya tukajenga jamii isiyo kua na maadili, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo”.

Akaendelea kufafanua kua: “Baadhi ya walimu hupata tabu katika nafsi zao wanapo chelewa kumaliza kusherehesha somo katika kitabu cha kufundishia kwa muda, wala hawaangalii upande wa kujenga muamala wenye maadili mema na wanafunzi jambo ambalo litawasaidia katika kufikia lengo (la kutoa elimu bora), yampasa mwalimu atambue kua ana nafasi kubwa sana ya kumuathiri mwanafunzi kitabia na kumfanya mwanafunzi azingatie masomo na awe makini kutokana na tabia ya mwalimu, kuamiliana kwema na maadili mazuri ndivyo vinatengeneza jamii yenye maondeleo”.

Akasisitiza: “Umuhimu wa kuweka msukumo katika kujenga tabia njema jambo hilo lipewa kipawa mbele na taasisi zote za elimu”. Mwisho alitoa wito kwa watu wenye mamlaka kutengeneza sheria itakayo walinda walimu.

Kisha alizungumza ustadh Karim Jaazii mwalimu wa malezi kutoka Bagdad, ambaye alisema kua: “Hakika ikhlasi katika kazi na kutekeleza wajibu vizuri pamoja na elimu ndio msingi wa maendeleo na ustaarabu wa umma, dini yetu ya kiislamu ni maarifa, elimu na malezi vinapata mabadiliko ya haraka sana katika dunia kushinda vitu vingine, lazima tujipanue katika upande wa malezi ikiwa ni pamoja na kuipa umuhimu maalumu sekta hiyo”.

Kisha akazungumza Muutamad Marjaiyya dini wa juu kutoka katika mji wa Raswaafa Shekh As-adi Zubaidi, akazungumzia umuhimu wa kuipa nafasi kubwa sekta ya elimu na malezi, na kuhakikisha zinapatikana njia nzuri za kusimamia swala hilo katika mazingira haya ambayo dunia inakasi kubwa ya maendeleo katika kila sekta.

Kikao kilihitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki kwa washiriki wote, na vinatarajiwa kuendelea vikao kama hivi kwa kushirikisha makundi mengine ya elimu kutoka Bagdadi au katika mikoa mingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: