Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) baada ya kufariki baba yake (s.wa.w.w) hakubakia duniani ispokua siku chache zilizojaa huzuni msiba na matatizo ya kila aina, hakuna aneyejua ukubwa wa matatizo hayo ispokua Mwenyezi Mungu, bibi Fatuma (a.s) alipo karibia kufariki alilala katika tandiko lililo kua katikati ya nyumba, akalala chali akiwa ameelekea kibla. Inasemekana: aliwatuma binti zake Zainabu na Ummu-kulthimu waende katika nyumba za ndugu zao (banii Hashim) ili wasishuhudie kifo cha mama yao, hii yote kwa ajili ya kuwapenda na kuwaonea huruma wasipate mshituko wa kushuhudia kifo.
Imamu Ali, Hassan na Huseein (a.s) nao walikua nje ya nyumba wakati huo, yawezekana kua kwao nje kulikua na hekima za Mwenyezi Mungu, imepokewa kua; wakati bibi Fatuma (a.s) alipokaribia kufariki alimuambia Asmaau kua: (Hakika Jibrilu alimjia mtume (s.a.w.w) –alipo karibia kufariki- akiwa na kafuur kutoka peponi, akaigawa sehemu tatu, sekemu ya kwanza yake mwenyewe na ya pili ya Ali na ya tatu sehemu yangu na zilikua dirham arubaini) kisha bibi Fatuma (a.s) akasema: (Ewe Asmaau niletee mafashi ya mzazi wangu yaliyo bakia yapo sehemu kadha na kadha na uniwekee kichwani kwangu), akachukua na kumuwekea baada ya kutawadha kwa ajili ya swala akamuambia: (niletee marashi ambayo hua najipaka na nguo ambayo hua naswalia), akajipaka marashi na akavaa nguo yake kisha akasema: (Nipe nafasi kidogo kisha baadae utanita, nisipo kuitikia ujue nimesha enda kwa baba yangu, utume taarifa kwa Ali).
Ulipo fika wakati wa ihtidhaar (kukaribia kukata roho) zikafunguka pazia bibi Fatuma (a.s) aliangalia kwa nguvu kisha akasema: (Amani iwe kwako ewe Jibrilu, amani iwe kwako ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, Ewe Mola pamoja na mtume wako, ewe Mola katika ridhaa yako na ujirani wako na mji wako mji wa amani), kisha akasema: (Huu ni msafara kutoka mbinguni na huyu hapa Jibrilu na huyu mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: Ewe mwanangu njoo kilicho mbele yako ni bora kwako) akafumbua macho yake na akasema: (Wa alaika salaam ewe mtoa roho fanya haraka wala usiniadhibu) kisha akasema: (Naja kwako Mola wangu sio katika moto) kisha akanyoosha mikono yake na miguu yake, Asmaau akamwita hakumuitikia, akamfunua usoni kwake akakuta tayali amesha fariki, akamkumbatia kwa kumbusu huku akisema: Ewe Fatuma utakapo fika kwa baba yako mtume wa Mwenyezi Mungu mfikishie salamu kutoka kwangu Asmaau bint Umais, kisha akaingia Hassan na Hussein wakamkuta mama yao amelala wakasema: Ewe Asmaau kitu gani kinamlaza mama yetu katika muda huu? Asmaau akasema: Enyi watoto wa mtume wa Mwenyezi Mungu mama yenu haja lala, bali ameaga dunia.
Hassan akamkumbatia huku anambusu na kusema: (Ewe mama yangu nizungumzishe kabla roho yangu haija tengana na muili), naye Hussen akawa anabusu mihuu ya mama yake huku anasema: (Mimi ni mwanao Hussein nizungumzishe kabla muyo wangu hauja pasuka na nikafa).
Asmaau akawaambia: Enyi watoto wa mtume wa Mwenyezi Mungu nendeni kwa baba yenu Ali mkamuambie kufariki kwa mama yenu, wakatoka hadi walipo fika karibu na msikiti sauti zao za kulia zikawa juu, wakafatwa na kundi la maswahaba wakauliza kitu gani kinawaliza, wakasema: (Amefariki mama yetu bibi Fatuma (a.s)). Imam Ali (a.s) akajipiga usoni kwake huku akisema: (Azaa ya nani ewe bint wa Muhammad?)..