Miongoni mwa ratiba za Atabatu Abbasiyya tukufu za kuhuisha minasaba ya Ahlulbait (a.s) ya mazazi na vifo (wilada na wafati) na kukumbuka matatizo na dhulma walizo fanyiwa, ambampo kufariki kwa bibi fatuma (a.s) hupewa umuhimu mkubwa, Atabatu Abbasiyya tukufu ilihuisha tukio hili la kusikitisha ambalo tupo katika siku zake kwa mujibu wa baadhi za riwaya zinazo sema ilikua ni tarehe kumi na tatu Jamadil Ula (siku 75) baada ya kufariki kwa mtume (s.a.w.w).
Kwa kufanya maukibu ya azaa ya pamoja baada ya Adhuhuri ya siku ya Juma Mosi ya tarehe (13 Jamadil Ula 1438h) sawa na (11/02/2017m) iliyo tanguliwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la wajumbe wa kamati ya uongozi na baadhi ya viongozi. Walipokelewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu halafu ikafanyika majlisi ya taaziya katika uwanja wa haram ya imamu Hussein (a.s) na kusomwa kaswida na mashairi ya huzuni yaliyo amsha hisia za huzuni katika nyoyo za watu kwa kukumbuka yaliyo jiri kwa Ummu Abiiha na kipenzi cha mtume (s.a.w.w) hasa baada ya kufariki kwa baba yake (s.a.w.w) na namna alivyo tenzwa nguvu na kuishi akiwa na hasira dhidi ya wale walio dhulumu haki yake.
Wakati wa matembezi zilisomwa beti za mashairi zilizo elezea tukio la msiba ulio umiza nyoyo za waislamu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wakapiga vifua vyao (maatam) kutokana na uchungu wa mambo yaliyo jiri kwa kipande cha nyama ya mtume mtukufu bibi Fatuma (s.a.w.w).
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba ya taaziya iliyo jumuisha mambo mengi ikiwemo utoaji wa mihadhara ya kidini, na kufanyika majaalisi za huzuni kwa ajili ya kuhuisha msiba huu, pamoja na kuweka mpango wa kupokea vikundi (mawaakibu) za azaa kutoka ndani na nje ya Karbala tukufu, wanao kuja kufanya taazia kwa imamu Abuu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).