Chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni tunu.. kituo cha msafara na wanazuoni) kongamano litafanyika tarehe (5-7/04/2017m) kwa mara ya kwanza linafanyika kongamano na maonyesho ya aina hii katika nchi ya Iraq chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tunatoa wito kwa watafiti na wabunifu wote waje washiriki katika maonyesho haya kwa kuonyesha ubunifu wao walio jaliwa na Mwenyezi Mungu katika sekta tofauti; sekta ya tiba, uhandisi, kilimo, na usalama (jeshi).
Kongamano hili na maonyesho yanalenga mambo yafuatayo:
Kwanza: Kusaidia na kushajihisha akili za wairaq katika kubaini vipaji vya wabunifu.
Pili: Kuchangia katika kujenga ari ya utafiti na ubunifu na kuileta katika uhalisia wa kitu kinacho onekana na kuchangia kufikia malengo ya kiubunifu sawa yawe ya muda mfupi au mrefu.
Tatu: Kunufaika na ubunifu wa wataalamu wetu na kuingiza ubunifu wao katika soko la ajira.
Nne: Kuchangia katika kuboresha uchumi wa Iraq kwa kuwatumia wabunifu wa ndani katika kuendesha miradi.
Tano: Kuingiza mafanikio ya ubunifu wa wataalamu wetu katika hatua ya utekelezaji kitaifa.
Sita: Kunufaika na wabunifu wa sekta ya viwanda, na kuingiza katika teknolojia ya uzalishaji.
Saba: Kujenga uelewa katika jamii kuhusu umuhimu wa wabunifu na ubunifu wao.
Kutakua na kongamano lingine siku za mbele ambalo litakua kama jukwaa la wabunifu kutoka pande zote za nchi hii, ambapo wataeleza fikra zao na kutoa nafasi ya kushirikiana kwa manufaa ya kujenga uchumi wa nchi kutokana na ubunifu wao utakao changia katika hazina ya teknolojia.
Mwisho wa kupokea taarifa za washiriki wa kongamano hili ni: (25/02/2017m) na tangazo la wabunifu watakao pasishwa kushiriki litatolewa tarehe (15/03/2017m), na namna ya kuomba kushiriki unatakiwa kujaza fomu maalumu iliyopo katika mtandao wa Alkafeel ( https://alkafeel.net/ifi) na kuituma katika email zifuatazo: Aiexcon2017@gmail.com au Scahc155@yahoo.com
kwa maelezo zaidi piga namba zifuatazo: (07700478333) au (07813764052) au (07730907902).