Kitivo cha masomo ya kibinadamu chahuisha kumbukumbu ya shahada ya bibi Zaharaa (a.s) kwa kufanya majlisi ya taazia..

Maoni katika picha
Idara ya lugha katika kitivo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya taazia, iliyo hudhuriwa na jopo la walimu wa chuo, wakiongozwa na mkuu wa chuo hicho dokta Swafaau Abduljabaar Ally Mussawiy na mkuu wa idara ya lugha Ustadh Mahmudu Swabbaar pamoja na wanafunzi wa chuo, katika majlisi hiyo walikumbuka kufariki kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Majlisi ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur’an tukufu kisha ukafuatia muhadhara uliotolewa na Sayyid Ammaar Ghuraifi kutoka Baharain, alizungumzia mambo mengi ikiwa pamoja na uhai wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na mambo yaliyo msibu miongoni mwa kudhulumiwa na kunyanyaswa baada ya kufariki kwa baba yake mtume Muhammad (s.a.w.w) na namna alivyo pambana na matatizo hayo kwa kusubiri na kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu, pia aliwahimiza wanafunzi kuiga mwenendo wake mtukufu na wadhihirishe kudhulumiwa kwake (a.s), wafasiri kauli zake na nasaha zake kwa kufanyia kazi halisi.

Majlisi ilimaliziwa kwa kusomwa mashairi yaliyo elezea tukio hili lenye kuumiza na yaliyo jiri kwa Ahlulbait (a.s) baada ya kufariki kwake (bibi Fatuma a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba ya taaziya iliyo jumuisha mambo mengi ikiwemo utoaji wa mihadhara ya kidini, na kufanyika majaalisi za huzuni kwa ajili ya kuhuisha msiba huu, pamoja na kuweka mpango wa kupokea vikundi (mawaakibu) za azaa kutoka ndani na nje ya Karbala tukufu, wanao kuja kufanya taazia kwa imamu Abuu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: