Kwa ajili ya kufungua milango ya kusaidiana na kushirikiana, ujumbe wa viongozi wa juu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu umekwenda kutembelea taasisi za kisekula na vituo vya kitafiti katika nchi ya Iran.
Ujumbe huo uliongozwa na rais wa kitengo hicho Shekh Ammaar Hilali na mkuu wa kituo cha turathi cha Karbala na mkuu wa kituo cha Basra na Hila pamoja na msaidizi wa mkuu wa taaluma wa kitengo hicho, ujumbe huu umetembelea taasisi nyingi na kujadiliana nazo kuhusu namna ya kushirikiana kwa manufaa ya wote, na kwa upande mwingine wameelezea kazi zinazo fanywa na kitengo chao katika sekta mbalimbali.
Ujumbe huu ulikua na vituo vingi, kituo cha kwanza kilikua katika mji mtukufu wa Qum, pia walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya imamu Ali (a.s) ndani ya mji wa Qum, na wakaangalia maendeleo yao katika utunzaji wa vifaa kale na vitu vya nadra walivyo navyo, wakasikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa makumbusho hayo.
Kisha wakatembelea chuo kikuu cha dini na madhehebu kilichopo katika mji mtukufu wa Qum, nacho ni miongoni mwa vyuo vya aina yake duniani vya masomo ya juu, ambapo ujume ulifanya kikao cha pamoja na rais wa chuo hicho Sayyid Abulhassan Nuwaab na mshauri mkuu wa chuo Sayyid Masjidi Jaamii, katika kikao hicho walijadiliana namna ya kusaidiana na kushirikiana katika mambo yanayo wajumuisha na wakasisitiza jarida linalo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu liandike kuhusu tafiti zao.
Pia wajumbe walipata fursa ya kutembelea maktaba ya taifa katika chuo kikuu cha Tehran, ambapo walikagua nakala kale na turathi za kiislamu zinazo rejea katika vipindi tofauti, mkuu wa maktaba hii alipo sikia vitu vilivyopo katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu na teknelojia wanayo tumia katika utunzaji wa vitu hivyo alionyesha moyo wa kutaka kushirikiana nao katika mambo yanayo wajumuisha.
Hali kadhalika walifanya kikao na mkuu wa kituo cha uhakiki wa tafiti kuhusu Qur’an tukufu katika wizara ya elimu na uhakiki ya Iran, katika kikao hicho walijadili nukta za kushirikiana katika kuhifadhi turathi za Karbala, Basra na Hila pamoja na turathi zote zilizopo katika ulimwengu wa kiislamu, na kuongeza ushirikiano na taasisi za utafiti kwa ajili ya kuendeleza turathi na kuangalia namna ya kubadilishana uzoefu kati ya vituo vya turathi vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi za kielimu na kitamaduni za Iran, na kufanya vikao vya kitafiti vya pamoja na makongamano ya kielimu baina ya pande mbili, pembezoni mwa kikao hiki, kilifanyika kikao kingine na muwakilishi wa wizara ya elimu na uhakiki ya Iran, dokta Hussein Salari Aamiliy, aliupokea kwa furaha ujumbe huu na akaonyesha utayari wa wizara kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta tofauti za elimu na kuboresha mawasiliano baina ya pande mbili.
Vile vile walimtembelea muhakiki mkuu na rais wa wahariri wa jarida la Basaataini linalo andika habari za turathi Sayyid Mutaqi, wakajadiliana kuhusu njia mpya za kuhakiki nakala kale.
Halafu ugeni ukatembelea chuo cha Aabaad ndani ya chuo kikuu cha Tehran na wakafanya kikao na mkuu wa chuo hicho pamoja na baadhi ya walimu, Shekh Ammaar Hilali alipata nafasi ya kuelezea shughuli zinazo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu pamoja na idara zake na machapisho yake pamoja na mafanikio yaliyo patikana toka kuanzishwa kwake, kisha wakajadiliana fursa za kusaidiana na kushirikiana baina yao, naye mkuu wa chuo alionyesha utayari wake, na kua yupo tayali kutoa ushirikiano wa juu kabisa katika kufanikisha swala hilo, mwisho wa ziara hii ugeni ulitembelea maktaba ya chuo hicho na kufahamu vitu mbali mbali vilivyomo.