Wakina Fatuma wafanya taaziya kwa imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya shahada ya mama yake Zaharaa (a.s)..

Maoni katika picha
Kongamano la siku kumi za Faatwimiyya (Msimu wa siku kumi za huzuni ya Faatwimiyya) zinazo fanywa na kitengo cha minasabaati na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu vilivyo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kuanzia tarehe (11-21 Jamadil Ula) kila mwaka, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ilihusisha ratiba tofauti, ikiwemo kuandaa matembezi ya wanawake katika siku ya mwezi kumi na tatu Jamadil Ula.

Katika matembezi hayo walishiriki watu wenye majina ya Fatuma katika kutoa taazia ya wajina wao kipenzi wa mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), matembezi hayo yalianzia katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yakitanguliwa na jeneza la maigizo lililo bebwa na wakina mama ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kumaliza ratiba yao katika Atabatu Abbasiyya tukufu walitoka na kuelekea katika malalo ya Abul-ahraar imamu Hussein (a.s) kwa kutumia uwanja wa katikati ya haramu mbili tukufu (maa baina haramaini), walipo fika katika malalo matakatifu ya Abuu Abdillahi Hussein (a.s) zilisikika sauti za vilio wakati wa kuingia kwao katika uwanja wa haram ya imamu Hussein (a.s) kutoka kwa watu wanaokuja kufanya ziara (mazuwaru) walio shiriki matembezi hayo, wakikumbika yaliyo jiri na kumpata pande la damu ya mtume mtukufu (s.a.w.w) miongoni mwa dhulma na kudhalilishwa baada ya kufariki kwa baba yake (s.a.w.w) na namna alivyo tenzwa nguvu na akaishi katika hali ya hasira dhidi ya watu walio dhulumu haki yake.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba ya azaa iliyo husisha vitu vingi, ikiwemo utoaji wa mihadhara ya kidini, na kufanya majaalisi maalumu kwa ajili ya kuhuisha tukio hili, pia walitangaza utayali wao wa kupokea vikundi vya taazia (mawaakibu) kutoka ndani na nje ya Karbala tukufu, wanao kuja kutoa taazia kwa imamu Abuu Abdillahi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: