Majlisi ya maombolezo: Masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakumbuka msiba wa bibi yao Zaharaa (a.s)..

Sehemu ya majlisi
Kama ilivyo kawaida yao kila mwaka, masayyid watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya majlisi ya maombolezo ya bibi yao Fatuma Zaharaa (a.s) katika kumbu kumbu ya shahada yake, kumbukumbu hizi zimeacha huzuni ya kudumu katika nyoyo isiyo isha karne na karne, wataendelea kumlilia wajukuu na wapenzi wake, majaalisi hizi za maombolezo ni moja kati ya kuhuisha tukio hili ambalo hufanywa kila mwaka toka miaka saba iliyo pita.

Majlisi ya taaziya inafanywa alasiri ya kila siku katika Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia siku ya shahada yake (13 Jamadil Ula) na inaendelea siku tatu,hadi (15 Jamadil Ula); huanza kwa Qur’an tukufu kisha hufuatia muhadhara wa kidini halafu husomwa mashairi ya husseiniyya.

Mimbari ya azaa mwaka huu imepandwa na Sayyid Mudhir Kazwiniy kutoka katika kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kubainisha dhulma aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s) baada ya kufariki kwa baba yake mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na akasema; kumkumbuka kwake (bibi Fatuma a.s) tuna pata mazingatio makubwa katika maisha yetu na somo ambalo linatuangazia na kutuongoza kizazi baada ya kizazi, pamoja na kufahamu utukufu wa pekee alionao bibi Zaharaa (a.s) kwa baba yake mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). kisha humalizia kwa kusoma nauha (kaswida) za huzuni, ambazo husomwa na Sayyid Badriy Maamitha kutoka katika idara ya masiyyid watumishi katika Ataba.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba ya azaa iliyo husisha vitu vingi, ikiwemo utoaji wa mihadhara ya kidini, na kufanya majaalisi maalumu kwa ajili ya kuhuisha tukio hili, pia walitangaza utayali wao wa kupokea vikundi vya taazia (mawaakibu) kutoka ndani na nje ya Karbala tukufu, wanao kuja kutoa taazia kwa imamu Abuu Abdillahi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: