Kituo cha maarifa ya Qur’an tukufu kuifasiri na kuichapisha chaendesha semina ya awamu ya tatu na chasisitiza kuendelea kwa semina hizi..

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Qur’an tukufu kuifasiri na kuichapisha kilichopo ndani ya Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kimetangaza kufanyika kwa semina ya kujenga uwezo awamu ya tatu iliyo fanyika kwa anuani isemayo (Namna gani utaandika utafiti wa kiqur’an katika mwenendo wa vizito viwili) semina hii ilisimamiwa na tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu katika mji wa Sha’ab huko Bagdad, pia semina hii ililenga kutambulisha mashindano yaliyo tangazwa siku za nyuma, na washiriki wamesisitiziwa kushiriki katika mashindano hayo, na wakapewa kanuni za msingi katika kuandika tafiti hizo.

Mkufunzi wa semina na mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an tukufu kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau Dini Zubaidiy alisema kua: “Hii ni miongoni mwa semina nyingi ambazo zimesha fanyika katika mkoa wa Karbala na maeneo mengine, na Bagdad ni moja kati ya vituo vya semina hii, hizi kozi zinalenga kuonyesha umuhimu wa kuvifanyia kazi vizito viwili, na kubainisha umuhimu wa kushikamana navyo kwani ndio njia ya uongofu na haki. Katika semina hii imeshiriki idadi kubwa ya walimu, watafiti na wanafunzi wenye kutilia umuhimu masomo ya Qur’an kutoka katika miji tofauti ndaji ya mkoa wa Bagdad.

Akaendelea kusema kua: “Darasa hufanyika kila siku ya Ijumaa baada ya swala ya magharibi na ishaa kwa muda wa masaa matatu na litaendelea hadi wiki saba, husomeshwa kanuni za msingi katika uandishi wa tafiti na misingi ya kielimu maarufu katika sekta hii kwa muhtasari, pamoja na kubainisha lengo kuu la semina ambalo ni mwenendo wa vizito viwili Qur’an na kizazi kitakasifu”.

Shekh Zubaidiy akaendelea kusisitiza kua: “Sisi tutaendelea kufanya semina hizi kutokana na ratiba yetu na katika sehemu zilizo pangwa kwa kuangalia uwiano wa upatikanaji wa washiriki”.

Kumbuka kua kituo hiki kimesha fanya semina nyingi na nadwa za kielimu kuhusu Qur’an pamoja na kubainisha mwenendo wa vizito viwili, na imeandaa anuani zifuatazo kwa ajili ya kujibu swali lolote linalo husu semina zake na jambo lolote kuhusu Qur’an tukufu:

Barea pepe: m.t.t.q313@gmail.com

Namba ya simu: 07602323733 unaweza kupiga moja kwa moja au kutumia mitandao ya kijamii (face book, whatsap, viber na telegram).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: