Kupitia hema la Scout: Wanafunzi wa kitengo cha uchunguzi wa kiuguzi katika chuo cha masomo ya kibinadamu wafanya mamia ya vipimo kwa mazuwaru wa Ataba mbili tukufu..

Maoni katika picha
Wanafunzi wa kitengo cha uchunguzi wa kiuguzi katika chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kupitia hema la Scout lililo wekwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu wamefanya mamia ya vipimo kwa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) kwa Abuu Abdilahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa kama sehemu ya kukumbuka shahada ya bibi Zahara (a.s), wametumia fursa hii ya kupatikana kwa idadi kubwa ya mazuwaru wanao kuja kutokana na mnasaba huu kutoa huduma zao za kiuguzi kama sehemu yao ya kushiriki katika msiba huu mkubwa.

Program hii iliyo fanyika katika uwanja wa baina ya haram mbili tukufu ilihusisha vipimo tofauti, ikiwa ni pamoja na; kipimo cha damu, sukari, kuelewa group la damu pamoja na utoaji wa ushauri nasaha na maelekezo ya kitibabu, kwa ajili ya kujenga uwelewa wa kulinda afya kwa mazuwaru, na kunufaisha idadi kubwa ya watu wanao kuja kufanya ziara katika sehemu hii tukufu.

Watu walio kuja kufanya ziara (mazuwaru) wamesifu sana program hii na wameomba ifanyike mara kwa mara hasa katika misimu ya ziara za milionea (zinazo hudhuriwa na watu wengi) ambazo hushuhudiwa katika Ataba za Karbala tukufu.

Kumbuka kua hema la Scout lililo wekwa na chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu lilidumu kwa muda wa siku tano, na lilihusisha mambo mengi (kitaaluma, dini, tamaduni, na michezo) ikiwa ni miongoni mwa sehemu za harakati za kitengo cha malezi, kwa lengo la kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: