Balozi wa Ujerumani atembelea hospital ya rufaa Alkafeel na asifu huduma zake na kusema inamaendeleo makubwa..

Sehemu ya ziara
Balozi wa Ujerumani nchini Iraq bwana (Frantis Yuzif Karimbo) pamoja na ujumbe alio fatana nao siku ya Juma Nne ya tarehe (16 Jamadil Ula 1437h) sawa na (14/02/2017m) ametembelea hospititali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Alipokelewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na viongozi wa hospitali, ugeni huo ulitembelea vitengo na idara za hospitali, na walipewa maeleza kwa ufupi ya huduma za kibatibabu zinazotolewa na hospitali hii, pamoja na zana za kisasa inazomiliki hospitali katika sekta ya upasuaji na zinginezo.

pia kulikua na kikao cha utambulisho, ambacho viongozi wa hospitali walimuelezea balozi malengo ya kuanzishwa kwa hospitali hii, na kubwa zaidi ilikua ni kuchangia katika kuziba pengo la upungufu wa huduma za kimatibabu hapa Iraq.

Mwisho wa ziara balozi alitoa shukrani kwa viongozi wa hospitali na watumishi wake, akaonyesha kufurahishwa kwake na kile alicho kiona na kukisikia katika ziara yake hii, akasema kua hospitali inamaendeleo makubwa na inakidhi sifa za hospitali za kimataifa, akasema kua yupo tayali kufungua milango ya ushirikiano baina ya taasisi za afya za Ujerumani na hospitali ya rufaa Alkafeel, na kutoa ushirikiano unaohitajika wa kitaalamu au vifaa tiba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: