Kuendelea kwa maandalizi ya maonyesho ya kimataifa ya kumi na tatu katika mji wa Karbala..

Maoni katika picha
Tangu miezi mitatu iliyo pita kamati ya maonyesho ya vitabu ambayo hufanywa sambamba na kongamano la Rabiu Shahada inaendelea na maandalizi ya maonyesho ya kumi na tatu, imefanya mikutano na mazungumzo na taasisi zitakazo shiriki katika maonyesho hayo za ndani na nje ya Iraq kufatia masharti na kanuni za ushiriki zilizo tangazwa.

Kufatia maandalizi yanayo endelea; mkuu wa maonyesho hayo na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabii Shahada la kumi na tatu Sayyid Muyassir Hakim aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maandalizi yalianza miezi mitatu iliyo pita tumesha pokea baadhi ya washiriki kupitia mtandao, baadhi ya wasambazaji wametuma barua katika mtandao ili tuzipitie mara tu baada ya kufungua milango ya ushiriki”.

Akaendelea kusema kua: “Hadi sasa tumesha pokea maombi kutoka katika nchi mbalimbali, miongoni mwa nchi hizo ni: Lebanon, Jodan, Misri, Iran, na Iraq, tumesha anza kupitia maombi hayo chini ya kamati maalumu na kuandaa mazingira ya ushiriki, tunatarajia kukamilisha kila kitu mwezi mmoja kabla ya kufunguliwa kwa maonyesho, ufunguzi wa maonyesho ya mwaka huu utakua tarehe (24 mwezi wa nne) na yatadumu kwa siku (15)”.

Akafafanua kua: “Maonyesho ya mwaka huu yatakua na vitu vipya katika nyanja za washiriki na mpangilio pamoja na hata vitu vitakavyo onyeshwa”.

Kumbuka kua maonyesho yaliyo pita, taasisi zilizo shiriki zilikua (211) za ndani na nje, jumla ya nchi (13) zilishiriki ambazo ni: (Lebanon, Misri, Jodan, Umoja wa falme za kiarabu, Sirya, Moroco, Baharain, Saudi Arabia, Iran, Ungereza, Hispania, Canada, Itali pamoja na mwenyeji wao Iraq) ukubwa wa uwanja wa maonyesho ulikua karibia mita za mraba (3000), maonyesho yalihusisha maelfu ya vitamu na mada, ndani ya muda wa siku kumi za maonyesho kulikua na mafuriko makubwa ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: