Sayyid Swafi: Umma ulioe elimika ni umma hai umma usio ibiwa, hili ni muhimu sana turathi zetu zisiibiwe na kunufaisha wengine..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) kupitia khutuba aliyo itoa katika kongamano la kielimu la pili kuhusu faharasi na usanifu lililo endeshwa na kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumati kilicho chini ya ofisi ya Daru makhatutwati katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo siku ya Alkhamisi 18 Jamadil Ula 1438h sawa na 16/02/2017m chini ya kauli mbiu isemayo (Faharasi ni zana katika jamii ya waarabu kwa kutumia program ya RDA) kongamano litachukua siku mbili na litahusu umuhimu wa kuhifadhi turathi.

Akasisitiza kua: “Hakika watu wa kale pamoja na mazingira magumu waliyo kua wakiishi lakini walifanya juhudi kubwa kwa ajili ya kutufikishia maalumati kama zilivyo tufikia, kukawa na watu walio andika vitabu vingi na kukawa na maktaba kubwa zilizo jaa vitabu, kwabahati mbaya waislamu na waarabu wameishi katika matatiza ya vita, na miongoni mwa maeneo yaliyo kua yakilengwa na adui ni maktaba, hivyo maktaba zilikua zikichomwa kila baada ya muda fulani”.

Akaendelea kusema kua: “Uhifadhi wa turathi ni sehemu ya kuzifanya ziendelee kupatikana, kanuni za sasa zinataka kuendelea kubakisha turathi katika muonekano wake wa asili na kuhakikisha zinafikia kizazi kingine zikiwa katika muonekano uleule, faharasi zimetuhifadhia uhalisia wa athari za lugha ya kiarabu sawa sawa iwe katika vitabu vya kale au vya sasa katika mji wa Najafu, hakika vitabu hivyo vimechangia pakubwa katika nyanja ya elimu, baadhi ya vitabu vilikua katika hali nzuri na vinapatikana kwa urahisi, na baadhi ya vitabu vipo hadi leo lakini upatikanaji wake ni mgumu, kwa hiyo kuna umuhimu wa kuandiwa kwa faharasi zitakazo rahisisha upatikanaji wake”.

Akasema: “Faharasi za maktaba hii leo huchukuliwa kua ni katika elimu nzuri na fani muhimu sana, na baadhi za maktaba za sasa zinafanyia kazi swala hili katika upande wa usanifu au orodha ya vitabu walivyo navyo au aina zake, baadhi ya vitabu kila kinapo kuwepo katika orodha ndio inakua rahisi kukihifadhi na kinakua na thamani hata kama kitachapishwa mara nyingi”.

Akaendelea kusema kua: “Kuna mambo ambayo ni wajibu wetu sote, nayo ni kuhifadhi turathi, jambo hili lazima liandaliwe mazingira stahili, hapa katika Ataba tukufu maktaba yetu ilipata matatizo sawa na maeneo mengine ya kitamaduni hapa nchini, ilitelekezwa sana katika miaka ya nyuma, tulipo pata nafasi ya kuitumikia hatukukuta isipokua vitabu kale vichache vilivyo telekezwa sana, tulijitahidi kuboresha mazingira, hadi tumefikia nakala zaidi ya elfu tano katika elimu tofauti, baadhi ya vitabu kale (makhtutwati) kinakua kitabu kimoja katika nakala zaidi ya moja, kutokana na mwaka wa kuandikwa kwa kitabu, tukaingia katika hatua ya utibabu (urekebishaji) wa vitabu, tukapeleka jopo la watu katika nchi za ulaya kusomea swala hilo hadi wakapata vyeti vinavyo waruhusu kufanya kazi hiyo katika nchi za ulaya, kisha tukaweka faharasi ya maktaba na kazi bado inaendelea tumefikia hatua ya tatu katika kupanga faharasi ya vitabu kale, baada ya kumaliza hatua ya kwanza na ya pili, tulianza kuhakiki baadhi ya vitabu kale vilivyo andikwa kwa mkono, pia tumenunua mashine ya kuchapa vitabu ya kisasa, ambayo imechangia sana katika kulisha maktaba, hadi sasa tumesha chapisha zaidi ya nakala elfu moja za vitabu, na tumepanga kuchapisha nakala kale ya msahafu ulioandikwa kwa hati muiraq”.

Akasema: “Ulimwengu wetu wa kiarabu leo hii unaishi katika mtihani wa kuto jiamini na kujiona kua hatuwezi kua wabunifu, tatizo hili lina misingi yake, tunaishi tukisubiri watu fulani wagundue kitu ndio tufanye, kana kwamba kipaji cha ubunifu na ugunduzi tumenyang’anywa, wakati tunaweza kua wabunifu na wagunduzi kwa sababu tuna uwezo mkubwa sana, lazima tuwe na utashi tujiamini kua tunaweza kufika walipo fika watu wengine. Elimu na uwezo walio nao ndugu zetu wanaweza kua wagumduzi, jambo muhimu wasijidharau, kujidharau mwenyewe ndani ya nafsi yako kuna madhara zaidi kuliko kudarauliwa na mtu mwingine, kwa sababu mtu mwingine akikudharau unaweza kujirekebisha, waislamu tumeishi katika hali ya kudharauliwa, tukiangalia katika vita vya Uhudi waislamu walidharauliwa lakini wao walijiamini, na waarabu walipambana katika zama tofauti hadi wakafikia maendeleo makubwa, leo hii kutokana na elimu, uwezo na matashi tunatakiwa tufate nyayo za wazee wetu walio tangulia, pamoja na matatizo makubwa waliyo kutana nayo lakini waliweza kuandika vitabu vingi na wametuachia turathi tele”.

Leo tunajukumu la kimaadili katika utunzaji wa turathi zetu, hatutakiwi kuziangalia peke yake bali tunatakiwa kuzielezea ili zitusaidie katika kufahamu zaidi historia, sio sahihi mtu anapo simama katika turathi na kuondoka bila kufahamu zaidi yaliyo jiri kuhusu turathi hiyo, huko itakua ni kuzifanyia hiyana turathi zetu, lazima tunufaike nazo hadi mtu aseme sisi ni umma tunayo tuliyo kua nayo, kama walivyo tuanchia watu wa zamani turathi hizi na tunauliza walicho fanya watu wa miaka mia ya nyuma au zaidi na sisi tunajukumu la kuacha turathi kwa vizazi vijavyo na wataulizana kuhusu sisi, hivyo kuna umuhimu wa kuweka faharasi, jambo hili ni zuri kuthibitisha uwepo wetu na tuliyo yafanya tusije tukajitenga na ulimwengu.

Tupo wazi kwa kila fikra inayo kuja kutoka kwa mtu yeyote na tunafanya kazi kwa kuangalia uhalisia wa mambo, lengo la kongamano hili ni kubadilishana fikra na kunufaika na kila mtu, tunaamini kua uwezo unaendelea kuongezeka siku baada ya siku na maktaba zetu hazina tatizo la kutelekezwa tena kama zamani, bila shaka kwa kuto telekezwa kwake zinatoa mchango mkubwa sana wa elimu, na hakuna kitu chenye thamani kubwa zaidi ya elimu, pamoja na kua shahidi hupigana kwa muili wake na kumwaga damu yake lakini unakuta riwaya inasema, wino wa wanazuoni ni bora kuliko damu za mashahidi, umma wenye elimu ni umma ulio hai umma usio ibiwa, na hili ni muhimu sana; zisiibiwe turathi zetu na kuwanufaisha watu wengine, sisi tuna haki ya kuzitunza zaidi, na tunatakiwa kuelekeza nguvu zetu zote katika kuhudumia wasomaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: