Kufanyika kwa kikao cha kwanza cha kongamano la kielimu kuhusu faharasi na mpangilio wa maalumati..

Maoni katika picha
Katika ukumbi wa mikutano wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya leo siku ya Alkhamisi (18 Jamadil Ula 1438h) sawa na (16/02/2017m) kilifafika kikao cha kwanza cha kongamano la pili la faharasi na usanifu, linalo simamiwa na kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumati kilicho chini ya ofisi ya faharasi ni zana katika jamii ya waarabu na daru makhtutwati katika Atabatu Abbasiyya tukufu litakalo dumu kwa muda wa siku mbili na kuhudhuriwa na wataalamu wa ndani na nje ya Iraq.

Kikao hicho kiliongozwa na dokta Faiza Adib Abdulwaahid, mada ya kwanza ilitolewa na Ustadha Ghaada Damashqa iliyo kua na anuani isemayo; kanuni za kuelezea misingi (maswaadir) na kuiweka katika meza ya kimtazamo na kielimu.

Mada ya pili ilitolewa na dokta Azhaar Zaair Jaasim na dokta An’aam Zaair na mtandao wa RDA, walizungumzia utendaji kazi wa kanuni za kijamii na nafasi yake katika kuongeza uwezo wa faharasi. Mada ya mwisho ilitolewa na dokta An’aam Hussein na ilihusu athari za teknolojia katika utendaji wa kimaktaba, na akatumia mfano wa maktaba ya Hijri bun Adi katika chuo kikuu cha Mustanswariyya.

Tunapenda kukumbusha kua kongamano hili litaendelea kesho siku ya Ijumaa (19 Jamadil Ula 1438h) sawa na 17/02/2017h) asubuhi kutakua na mada mbili na jioni utafanyika ufungaji wa kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: