Sayyid Swafi asisitiza kua: Iraq sio nchi ya nyuma kwa sababu inarasilimali nyingi na uwezo mkubwa pia wairaq wana fikra pevu..

Maoni katika picha
Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amerejea kauli yake kua Iraq sio katika nchi zilizo baki nyuma, kwasababu inarasilimali nyingi na uwezo mkubwa pia wairaq wana akili pevu, daima narudia hii kauli.

Hayo aliyasema katika hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq iliyo fanyika alasiri ya Ijumaa (19 Jamadil Ula 1438h) sawa na tarehe 17/02/2017h, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tumezoea kila mwaka kuvitumikia vyuo vikuu vyetu vitukufu na nchi yetu kipenzi pamoja na walimu, na vijana wetu na mabinti zetu ambao tunatarajia kuwaona wakishindana katika kujenga nchi, hakika ni jukumu letu kuwafanyia kila kilicho ndani ya uwezo wetu”.

Akasema: “Tutakapo taka kumpa majukumu mtu yeyote lazima tuangalie wasifu wa mtu huyo kama anaweza kubeba majukumu hayo, jambo la kwanza: mtu mwenyewe, na sisi tunaamini kua wahudhuriaji wetu watukufu mnazo sifa, walimu mnawakilisha watu bora kabisa katika nchi hii, na wanafunzi ni miongoni mwa wanufaika wa kwanza wa elimu bora kutoka wa walimu inayo wabainishia majukumu yao,

Jambo la pili: kubainisha jukumu analo pewa mtu”.

Akaendelea kusema kua: “Ni muhimu kuangalia historia, ikiwa hatuwezi kuangalia yote basi ni muhimu kuangalia hata baadhi yake, na tuangalie kwa nini baadhi ya watu hufanikiwa na wengine hawafanikiwi, kuna sababu gani zinazo fanya umma usifanikiwe, kukosa maendeleo sio jambo zuri, ni miongoni mwa sifa mbaya, tunapo usifu umma kua hauna maendeleo hii ni sifa mbaya, Iraq sio katika Nchi zisizo kua na maendeleo kwa sababu ina rasilimali nyingi na uwezo mkubwa pia wairaq wana akili pevu, daima narudia nene hili ili kutilia msisitizo, ina uwezo wa kushinda mitihani, mlipo kua katika shule za msingi wakati mkiwa wadogo, Iraq ilikua inapita katika wakati mgumu sana, ilikua na matatizo mengi, tatizo hatutunzi historia yetu”.

Akasema: “Vizazi vijavyo wakiona ushahidi wa historia ulio tunzwa vizuri utawasaidia katika kujenga nchi, ili mtu aweze kuwajibika vizuri anatakiwa ajue vizuri jukumu lake, sasa hivi nyie wanafunzi mtabeba jukumu kubwa, mtafanya kazi katika maeneo muhimu ndani ya nchi hii, sawa iwe katika sekta za kiofisi, kisiasa, kiuchumi na kijamii, nyie mtakua ndio wenye maamuzi, maamuzi mtakayo fanya katika jambo lolote mtawajibika kwayo, lazima mpange uwajibikaji huo na namna mtakavyo fanya kazi zenu”.

Sayyid Swafi akawaambia wanafunzi kua: “Nchi inaumwa na sisi hatupendi kuuguza, mwanadamu anatakiwa afanye kazi kwa bidii hususan atakapo pata fursa hiyo, nchi inajifaharisha na nyie baada ya siku chache mtakua na nyadhifa muhimu katika nchi hii, maamuzi yenu yatakua na nafasi kubwa, hivyo lazima muwe na mtazamo sahihi wa kujenga, lazima mjiheshimu muwe imara msijidharau, pamoja na matatizo ya nchi na raia wake, mtu atakaye jiamini matatizo yote yatakua mepesi kwake, kinyume na mtu atakaye yaona mambo kwa ugumu na akajiona kua hayawezi kila kitu kitakua kigumu kwake, hili jambo ni muhimu sana kulifahamu (hakika hima huhuisha umma)”.

Akaendelea kusema: “Hakika tunafanya hivi ndugu zangu ili tushirikiane katika majukumu, inawezekana nafasi yangu ikawa ni kuongea na nafasi yako ikawa ni kutenda na kujenga na kuiambia batili, hapana! Nafasi yako ikawa ni kujitenga na rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma na ukawa unafanya kazi kwa ajili ya kujenga taifa”.

Akaendelea kusema kua: “Tunapo lalamikia tatizo fulani, haitoshi kutoa kasoro peke yake, bali inatakia tuonyeshe njia ya kurekebisha kama kuna jambo baya yapo mambo mazuri pia, inatakiwa nchi iwajali watu wake, hapa tunaona jambo baya la ufisadi pia kuna maeneo mengine masafi hayana ufisadi, kuna baadhi ya watumishi hawaja wahi kupokea mali ya haramu”.

Akasema: “Iraq leo hii inawahitajia sana na hali ni chanya lazima kuifanyia kazi, sisi tukitengeneza mazingira ya kuchukia rushwa watu wata achana nayo, lakini tukiifanya kua jambo la kawaida watu wataenelea nayo na itachangia kuendeleza ufisadi, hivi ndio alivyo ashiria imamu Ali (a.s) pale alipo sema: (Alituamrisha mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) tukutane na wafanya maasi kwa nyuso zenye hasira ili watu waache kufanya maasi)”.

Akaongeza kusema kua: “Sote tuna jukumu la kujenga nchi, narudia kusema kua; yawezekana nyie wakati mlipokua katika shule za msingi hamkuhisi matatizo kipindi hicho lakini sasa hivi mmeanza kuhisi majukumu, kuhisi kwako majukumu sasa hivi ujue kua tayali umesha ingia katika majukumu sasa angalia unafanya nini, je unaendelea kukosoa na kutoa kasoro kama ulivyo kua ukifanya siku za nyuma au unapambana kurekebisha hali kama ulivyo kua ukitamani?! Bila shaka sisi tuna amini kua mtatatua matatizo japo kidogo”.

Akasema: “Tengenezeni mazingira ya kukubali jambo zuri na kukataa jambo baya, msitangulize mali, mali zitakuja tu, mwanadamu anapo uza elimu yake huuza na nchi yake, ubinadamu wake na matashi yake, matashi yakiuzwa hauwezi kuyafidia kwa mali, mwanadamu anaye fikiria kuitumikia nchi yake ataona matunda yake baadae, hakika sisi tunaimani kubwa na vijana wetu, mabinti zetu tunakupeni pongezi nyingi sana, pokeeni pongezi hizi kwa kufanya kazi kwa bidii, mmekuja katika zama ambazo ufisadi umekithiri, msifuate kauli ya Mutanabii isemayo (Kilio cha wengi harusi) kauli hii sio sahihi, unatakiwa uwajibike katika kurekebisha maovu yaliyopo katika umma”.

Sayyid Swafi akamaliza kwa kusema: “Natoa tena shukrani kwa walimu watukufu wanao fanya juhudi kubwa katika ufundishaji, na kuwafanya wanafunzi wapate elimu bora, ninawaomba wawapende wanafunzi wao, mwalimu anapo mpenda mwanafunzi wake inamsaidia mwanafunzi katika kueliwa masomo na kuiga mazuri ya mwalimu wake, kwa sababu mwalimu ana nafasi kubwa sana katika kumuaathiri mwanafunzi, natoa shukrani pia kwa familia tukufu zilizo fanya kila lililokua ndani ya uwezo wao kwa ajili ya kuandaa mazindira ya kumuwezesha mtoto wao kua mwanafunzi bora, hakika wao wana nafasi kubwa katika nchi hii, kila kitu tunacho kifanya, tunafanya kwa ajili ya dini, dini ipo katika kila kitu, tutakapo wakabidhi vyeti yawezekana havina uzito wowote kimadda, lakini fahamuni kua mtakapo pokea vyeti hivi kwa mikono yenu mitukufu, hakikisheni mikono hiyo haishiki mali ya haramu –Allah awaepushe na hilo- vyeti hivi havikai pamoja na mali za haram”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: