Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza ushiriki wake katika vita vya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul ulioanza asubuhi ya siku ya Juma Pili (19/02/2017m) chini ya kauli mbiu ya (Tunakuja ewe Nainawa) ambapo watapigana bega kwa bega na vikosi vingine vya jeshi la serikali, habari zinasema kua tayali waliuvamia mji wa Arbidi na wakafanikiwa kukomboa maeneo ya milima ya Muhtariqa karibu ya kijiji cha Bakhira kutoka mikononi mwa Daesh na tayali wanayadhibiti maeneo hayo, hakika wapiganaji wana hamasa kubwa sana wamevaa ngao ya ujasiri na kujiamini wanasonga mbele kuwatimua magaidi wa kidaesh katika nchi.
Kumbuka kua ushiriki wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika vita hii ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul kunatokana na uzoefu mkubwa waliopata katika vita mbalimbali walivyo shiriki pamoja na vikosi vingine vya hashdi sha’abi na jeshi la serikali pamoja na vikosi vingine vya kujilinda, pia kutokana na mafunzo ya hali ya juu ya kivita waliyo nayo na moyo wa kujitolea unao tokana na imani yao kuhusu nchi hii kipenzi na kushikamana kwao na maelekezo ya Marjaa dini mkuu.