Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi ya Ataba tukufu na akapokea maelezo kutoka kwa watendaji wa miradi hiyo kuhusu ile iliyo kamilika na ambayo bado inaendelea, pamoja na hatua zilizo fikiwa ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu vikwazo vinavyo weza kujitokeza.
Ziara hii ni miongoni mwa ratiba yake ya kutembelea miradi na harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kukagua maendeleo, safari hii katembelea kituo cha tiba ya meno kilichopo katika jengo la Umulbanina (a.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika barabara ya Najafu – Karbala na akasikiliza maelezo kuhusu huduma zinazo tolewa na kituo hicho kutuka kwa watumishi wake, na mambo wanayo hitaji kusaidiwa.
Kisha alitembelea mradi wa chuo cha udaktari chini ya chuo kikuu cha Ameed, akakagua maendeleo ya ujenzi, rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Muhandisi Abbasi Mussa Ahmad alitoa maelezo ya kina kuhusu hatua za ujenzi huo na namna wanavyo jenga kutokana na idadi ya wanafunzi na aina ya vitengo vya masomo yatakayo fundishwa, naye Sayyid Ashiqar alitoa maoni yake ya kitaalamu ambayo yalipewa umuhimu mkubwa sana na watekelezaji wa mradi na wakaahidi kuyafanyia kazi, pamoja na hivyo alionyesha kufurahishwa kwake na namna ujenzi unavyo fanyika kwa kutumia njia za kisasa na akasifu kua mradi huu utakua mfano kwa miradi itakayo kuja.
Halafu katibu mkuu bamoja na watu alio fuatana nao ambao ni wajumbe wa kamati ya uongozi na viongozi wa idara za Ataba tukufu, wakaelekea katika mradi mwingine ambao upo katika hatua za awali za utekelezaji wake, nao ni mradi wa magodauni uliopa katika barabara ya Karbala – Ibrahimiyya, unaojengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (85,750) ambalo litajengwa godauni tatu kubwa kila moja ikiwa na ukubwa wa mita za mraba (2500) na kufatiwa na jengo la ghorofa mbili, kila ghorofa itakua na ukubwa wa mita za mraba (3,000), shirika linalo tekeleza mradi huu –Shirika la bendera ya kimataifa la biashara na ujenzi- lilitoa maelezo ya kina kuhusu maendeleo ya kazi za mradi huu na njia wanazo tumia katika ujenzi wao ikiwa ni pamoja na mbinu za kitaalamu na kihandisi wanazo tumia katika kufanikisha ujenzi huo.
Baada ya hapo Sayyid Ashiqar alielekea katika stoo ya Sajjad ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyopo katika jengo la Saqaau/1, akasikiliza maelezo kutoka kwa mtunzaji mkuu wa vifaa katika stoo hiyo na namna wanavyo tunza vifaa na taratibu za kuingiza na kutoa kifaa ndani ya stoo hiyo.
Akamalizia ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha maji cha Alkafeel ambacho ni miongoni mwa miradi ya uzalishaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu, akakagua utendaji wa kiwanda hicho na akapokea maelezo kuhusu uzalishaji wake na aina za maji yanayo zalishwa pamoja na aina ya mitambo wanayo tumia katika usafishaji na utunzaji wa maji, halafu akapitia katika kiwanda cha kutengeneza barafu.
Viongozi wa Ataba tukufu walisikiliza maelezo kuhusu kujiandaa kwa kiwanda hicho kwa ajili ya msimu wa joto ujao, naye katibu mkuu alisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi kwa watumishi wa miradi yote aliyo tembelea kwa ajili ya kuboresha huduma zinazo tolewa na Ataba tukufu kwa watu wanao kuja kufanya ziara.